WANANCHI WAMKATAA RASMI GAMBO ARUSHA WADAI NI MWONGO SANA,WAMTAKA MAKONDA PIA WATISHIA KUTOSHIRIKI UCHAGUZI KISA KIVUKO!

 Na Joseph Ngilisho -ARUSHA


WANANCHI wa Kata ya Sokon one,Jijini Arusha wameibua tafrani baada ya kujikusanya na kutishia kutopiga kura katika uchaguzi mkuu ujao wakiwa na madai ya kutaka kujengewa kivuko baada ya kuahidiwa kwa muda mrefu bila mafanikio.

Aidha wananchi hao wakiongea kwa jaziba wamemkataa mbunge wao Mrisho Gambo wakidai hajawasaidia chochote na kuahidi kutomchagua tena iwapo atagombea  nafasi hiyo ,kwa madai ya kushindwa kutekeleza ahadi yake ya kuwajengea kivuko baada ya kuwa akiwaahidi mara kadhaa bila kutekeleza hadi yake.

Walidai kwamba kivuko hicho ni muhimu sana kwa maendeleo yao kwani kimekuwa kiungo kikubwa kwa  wananchi zaidi ya 2000 wanaopita kila siku wakiwemo wanafunzi 300 na kuziunganisha kata tatu za Muret Sokon one na Lemara  zilizopo katika jiji la Arusha.

Walidai licha ya kumkataa mbunge wao pia wamemkataa diwani wa kata hiyo ,Saluni Olodi kwa madai ameshindwa kuwajengea kivuko hicho .

"Mrisho Gambo alikuja hapa na kutuahidi atatujengea daraja la chuma lakini hadi sasa hakuna kitu ,tumechoka kudanganywa kama watoto"

Wananchi hao walisikika wakipiga kelele wakisema hawatapiga kura iwapo serikali itashindwa kuwajengea kivuko hicho ikiwa ni njia moja wapo ya kushiniliza kujengwa kwa kivuko hicho muhimu kwa ustawi wa maisha yao ya kila siku.

Walidai kwamba Gambo aliamua kuwajengea kituo cha afya ili pindi wanapoanguka wakati wakipita katika kivuko hicho waende kutibiwa jambo ambalo wamesema wamechoka na hawataki kusikia danganya toto tena.

Balozi wa mtaa wa Muriet  Elibariki Mollel alisema kuwa kivuko hicho kilijengwa kwa nguvu za wananchi na  sasa kimekuwa hatarishi zaidi kutokana  na kuoza kwa kingo za mbao pamoja na magogo yaliyoezekwa na kusababisha watoto kudondoka na kuvunjika miguu wakati wakipita majira ya alfajiri kwenda shuleni.

"Watu wanaotumia kivuko hiki kila siku ni zaidi ya 2000 ,pia wanafunzi wanaovuka hapa kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine ni zaidi ya 300 ,wazazi wanalazimika kila siku alfajiri kuwavusha watoto wao wakihofia kudondokea mtoni wakati wanaenda shule, sasa hii ni kero ya muda mrefu sana ambayo wamechoka kuvumilia"Alisema Balozi.

"Mkuu wa mkoa Paul Makonda tunaomba utusaidie Mbunge hawezi kutusaidia amekuwa akitudanganya kama watoto"Alisema Mariam Juma mkazi wa muriet

Kwa upande wa diwani wa kata ya sokon one,Sarun Olodi alisema kuwa suala hilo linashughulikiwa ngazi ya halmashauri .Hata hivyo wananchi hao walishindwa kumsikiliza diwani huyo wakidaii amezidi  kwa uwongo uliopindukia.

"Ishu  hapa sio mbunge ama mkuu wa mkoa kuja hapa, ishu ni kivuko kujengwa"Alisikoka.diwani akisema huku wananchi walimzomea.






Ends..




Post a Comment

0 Comments