VIONGOZI OLOSIVA LAWAMANI KWA KUBOMOA KUTA ZA NYUMBA ZA WANANCHI BILA KUWASHIRIKISHA, WAIOMBA SERIKALI KUINGILIA KATI NA KUWACHUKULIA HATUA ZA KISHERIA!TAZAMA PICHA !

 Na Joseph Ngilisho ARUMERU 


WANANCHI zaidi ya 200 wakiwemo mabalozi,diwani na mtendani kata katika kitongoji cha Olosiva wilaya ya Arumeru wamejichukukia sheria mkononi kwa  kubomoa kuta za nyumba za zaidi ya 100 bila kuwashirikisha wahusika jambo linaloashiria uwepo wa uvunjifu wa Amani.

Tukio hilo kimetokea mwishoni mwa wiki na kuzua taharuki kubwa kwa wananchi waliobomolewa  kuta zao wakidai hawajashirikishwa juu ya mpango huo na wameiomba serikali ichukue hatua kwa matukio ya aina hiyo ili kuepusha usumbufu na hasara inayojitokeza.

Mkazi mmoja wa eneo hilo  Glori Maule ambaye ukuta wake wa nyumba umebomolewa ukiwa na thamani ya sh, milioni 15,alidai kuwa hakuwahi kushirikishwa juu ya uwepo wa mpango huo wa upanuzi wa barabara ila ameshangaa mapema akiwa kazini kwake kupata taarifa juu ya kubomolewa kwa ukuta wa nyumba yake .

Alisema ziezi hilo liliongozwa na diwani pamoja na afisa mtendaji wa kata Oloriel waliokuwa wakiwahamasisha wananchi kubomoa kuta zinazoonekana kuwa ndani ya eneo la barabara.

"Sisi hatukubaliani na bomoabomoa inayoendelea wametuvunjia kuta zetu bila taarifa tunaomba serikali iingilie kati hawa viongozi hawana kibali cha kubomoa nyumba zetu"Alisema  mwananchi ambaye ni mmoja ya waathirika wa zoezi hilo
Mkazi mwingine,Aliraza Mohamed alisema kuwa ameishi katika kitongoji hicho kwa miaka 30 akiwa anahati miliki ya eneo lake na kujenga ukuta hivyo kitendo cha viongozi kuwatumia wananchi kuvunja kuta za nyumba zao bila kuwanagirikisha sionsahihi.

"Kimsingi mimi kama mkazi wa miaka mingi katika eneo hili sikatai maendeleo  ya barabara maana hata mimi naitumia ila lazima wafuate taratibu za kubomoa kuta za nyumba za watu kwani hakuna aliyeko juu ya sheria"


Diwani wa kata hiyo ,Erick Samboja alisema kuwa zoezi hilo limetokana na maamuzi ya wananchi yaliyotokana na mkutano uliofanyika katika kata hiyo na miongoni mwa mambo yaliyozungumzwa na kuamuriwa ni suala na ubovu wa barabara.

"Hili jambo limeibuliwa na wananchi katika mkutano wa hadhara baada ya barabara hii kuwakero kubwa kwa muda mrefu na kuwesa wananchi  hasa wakati wa mvua zinaponyesha ,tuliamua kuwapa notisi wananchi juu ya uwepo wa zoezi la upanuzi wa barabara hiyo"

Mmoja ya viongozi waliokuwa wakisimamia zoezi hilo balozi,Michael Mollel alidai kwamba ,wananchi walikaa  kikao na kukubaliana kufanya upanuzi wa barabara hiyo ambayo imekuwa na changamoto kubwa ya kutopitika kirahisi wakati wa mvua ili kujenga mitaro iweze kupitia kirahisi na kuondoa adha ambayo imekuwa ikiwakumba.


Wakazi hao ambao wengi wao wahamiaji wameiomba serikali kuingilia kati ili utaratibu mzuri zaidi uweze kutumika ikiwemo kuwaashirikisha  kabla ya kubomka makazi yao.

Naye mwenyekiti wa kitongoji cha Olisiva  Loishie Kimani alisema tatizo la ubovu wa barabara ni la muda mrefu na kilio cha wananchi ni kuhusu upanuzi wa barabara pamoja na kuweka mitaro.

"Nimeingia madarakani na kukuta hili tatizo la ubovu wa barabara ila niliamua kulivalia njuga suala hili kwa kuwapatia barua wananchi wote ambao kuta zao zipo ndani ya barabara "

Wananchi waliovunjiwa kuta zao za nyumba wameiomba serikali kuingilia kati kwa kuwa wamepanga kuandamana kupinga zoezi hilo ambalo linawapa hasara kubwa baada ya viongozi kuwahamasisha wananchi kubomoa kuta za nyumba zao kwa madai ya kupanua barabara wakidai jambo hilo ni haramu kwa sababu tara wakala wa barabara mijini na vijijini TARURA haba taarifa.




Ends..








Post a Comment

0 Comments