TANPA WAJIFUNGIA ARUSHA KUBORESHA HUDUMA ZAO,DKT MPOKI AWATAKA KUBUNI MBINU MBADALA ZA KUPUNGUZA VIFO KWA WATOTO

 Na Joseph Ngilisho -ARUSHA 


CHAMA cha wataalamu watoa dawa za usingizi na Ganzi Tiba Tanzania ( TANPA) kimekutana mkoani Arusha kwa lengo la kujadili namna ya kuondoa changamoto zilizopo kwa wataalamu hao na kuweza kuboresha utoaji wa huduma  katika idara hiyo. 

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la  3 la kisayansi la wataalamu hao  linalofanyika jijini Arusha kwa siku 3,alisema kuwa lengo la kongamano  hilo ni kuweza kubadilishana mawazo na uzoefu na kuweza kupata uelewa zaidi katika maswala hayo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya tiba na mifupa na ubongo kutoka Muhimbili na Mlezi wa chama hicho Dkt Mpoki Ulusubisya  amesema ni wakati wa kubuni mbinu mbadala katika Afua za utoaji huduma na kupunguza vifo vya watoto wachanga huku asilimia 6 ikihusishwa na utoaji wa dawa za usingizi huku kukiwa na vitendekazi  hafifu .


Kwa upande wake Rais wa Chama cha wataalamu watoa dawa za usingizi na Ganzi Tiba  Tanzania ,Julia Mahemba  alisema kongamano hilo la  3 linalofanyika kila mwaka  limejumuisha madaktari wa usingizi, matabibu ,wauguzi na wakunga kutoka Tanzania bara na visiwani kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma bora ,salama za upasuaji na kutathmini utendaji kazi wao.

“kupitia kongamano hilo wataweza kutambua pia nafasi yao katika utoaji wa huduma hiyo kwani ni sekta muhimu sana nchini .”alisema Mahimba 

Aidha ametaja changamoto iliyopo ni uwepo wa wataalamu wachache katika maeneo ya utoaji wa huduma ya afya jambo ambalo.linafanya kazi hiyo kutofanyika vizuri.

Mmoja wa washiriki katika kongamano hilo  Daktari bingwa Venance Misago na Samweli Mushi amesema kuwa,kupitia kongamano wataweza kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi wao wa kila siku na kuweza kuokoa afya ya Mama na mtoto.

Walisema kuwa,wameweza kupata ujuzi wa kutosha katika kuhudumia.wakina mama wajawazito ambapo wameahidi kuendelea kujiendeleza kimasomo zaidi kwani uhitaji bado ni mkubwa .


Dkt Mushi amesema kuwa, kuna haja ya kuongeza wataalamu  hao kwani uhitaji bado ni mkubwa sana na kila mmoja anajua upasuaji hauwezi kufanyika bila kupewa dawa hizo hivyo kuna umuhimu mkubwa sana wa kuongeza wataalamu hao.

Ends..

Post a Comment

0 Comments