TAJIRI WA MADINI ARUSHA AFANYIWA BALAA ZITO NYUMBANI KWAKE AKALISHWA NDANI YA ZIZI LA NG'OMBE YEYE NA FAMILIA YAKE , WANANCHI WAFURIKA NYUMBANI KWAKE , DC ATIA TIMU AONDOKA NA NG'OMBE -TAZAMA PICHA HAPA!

Na Joseph Ngilisho-MONDULI

MAMIA ya wakazi wa Kijiji cha Moita Bwawani wilayani Monduli,Mkoa wa Arusha, wakiwemo viongozi wa kimila Laigwanani ,wamefurika nyumbani kwa Mfanyabiashara ,Sanare Mollel(Mullah )kwa lengo la kumpatia baraka za kimila pamoja na kuipongeza serikali kwa kufanikisha kurejeshwa eneo la malisho lililokuwa limeuzwa kinyemela na viongozi wa kijiji hicho wasiokuwa waadilifu.


Sherehe hizo za kimila zimefanyika alfajiri ya leo nyumbani kwa Mfanyabiashara  huyo katika zizi la Ng'ombe wakati mfanyabiashara huyo na familia yake wakiwa wameketi kwenye ngozi ya Ng'ombe na kuzungukwa na Ng'ombe akiwa anamwagiwa baraka kwa kutumia vibuyu maalumu vilivyokuwa na dawa maalumu inayoheshimiwa na kabila hilo la kimasai.


Wananchi hao wamemshukuru mdau huyo wa maendeleo mwenye familia ya wake wanne na watoto takribani 15 ,kwa kukataa kuuziwa Ardhi hiyo na kuonesha msimamo wake wa  kutaka kulikomboa eneo hilo na kulirejesha kwa wananchi kwa maslahi ya kijiji hicho na jamii ya wafugaji ambao wengi wao ni maskini wanaoishi kwa kutegemea ufugaji.


Mmoja wa Laigwanani,Kapei Yaro alisema kilichowakutanisha katika boma la Sanare ni kumshukuru kwa kukiheshimisha kijiji hicho kwa kufanikisha kurejeshwa kwa eneo la malisho na wao kama Laigwanani wanambariki kwa kumvalisha taji la heshima baada ya kumaliza kazi .


Pia wanampongeza Mkuu wa hiyo Festo Kiswaga kwa kumaliza mgogoro huo uliodumu kwa zaidi ya miaka sita baada ya kurejesha kwa wananchi eneo hilo lenye ukubwa wa ekari elfu 10 .

Laigwanani mwingine,Julias Saiboro alifafanua kuwa tukio lilifanyika kijiji hapo ni tukio la baraka ambalo jamii ya  Kimasai hulifanya kwa kumbariki mtu ama watu waliofanya jambo jema lenye maslahi kwa jamii.


"Kilichofanyika hapa leo ni kitendo cha baraka baada ya wananchi wa Moita kufurahi waliporudishiwa Ardhi yao iliyokuwa imeuzwa na leo tumekuja kumbariki Bwana Sanare aliyeshiriki kurejeshwa kwa eneo la malisho na kukataa kuuziwa"



Diwani wa Kata ya Moita,Prosper Meyani pamoja na kumshukuru mdau huyo wa maendeleo pamoja na wananchi wengine waliokuwa mstari wa mbele kupambania rasilimali hiyo ya kijiji,aliwataka wananchi kuendelea kuyalinda maeneo ya malisho na wasikubali kuona maeneo hayo yakiuzwa  kwa maslahi ya viongozi wachache wenye njaa zao .


"Nimpongeze mdau wa maendeleo ambaye leo wazee wa kimila (Laigwanani) wamembariki , niwaombe wananchi hasa sekta ya wafugaji kuendelea kuyalinda maeneo ya malisho kwa sababu yamesaidia kulinda kundi kubwa la watu maskini wanaoishi kwa kutegemea ufugaji"Alisema.


Wananchi hao wamempa heshima ya kuwa balozi wa kutetea maeneo ya malisho ,heshima ambayo ameipokea kwa mikono miwili na kuahidi kuitunikia bila woga.


Kwa upande wake Sanare Mollel (Mullah)aliwashukuru wananchi kwa kumbariki baada ya kutambua mchango wake katika kupigania Ardhi ambayo tayari ilishauzwa kwa watu mbalimbali na kuahidi kupokea nafasi aliyopewa ya kuwa balozi wa wafugaji .


"Kimsingi mimi niwashukuru sana wananchi kwa kunibariki baada ya kutambua mchango wangu maana mgogoro huo umechukua muda mrefu lakini nilipambana bila kuchoka na hatimaye serikali ilisikia kilio chetu na kurejesha kwa wananchi ardhi yao"Alisema.


Naye diwani wa viti Maalumu, Monduli,Mary Sanare alimpongeza rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea mkuu wa wilaya ya Monduli,Festo Kiswaga ambaye  ameweza kutatua mgogoro  huo kwa muda mfupi ,ambao uliwashinda wakuu wengi wa wilaya hiyo waliopita, huku chanzo chake ni viongozi wachache wenye kujali maslahi yao binafsi kuamua kuuza maeneo yaa malisho bila kufuata taratibu.


Mkuu wa wilaya ya Monduli ,Festo Kiswaga ametoa onyo kali kwa viongozi wa vijiji ambao wamekuwa na tabia ya kuuza maeneo ya malisho akidai kwamba fedha hizo watazitapika na Ardhi itarudi kwa wananchi.


Alisema amegundua mbinu mpya iliyobuniwa na viongozi wa kijiji kuuza ardhi za malisho ,ambapo alidai wanatumia mpango mpya wa kugawa maeneo ya wazi kwa wananchi kwa nakubaliano maalumu na baada ya muda fulani eneo hilo huuzwa na fedha hizo hugawana.


"Viongozi wa kijiji wamebuni mbinu mpya ya kuuza maeneo ya wazi wakijifanya kuyagawa kwa mwananchi na baadaye eneo hilo huuzwa na pesa kugawana ,sasa ole wake mwananchi atakayepewa eneo na kuliuza"Alisema


Dc Kiswaga aliapa kuwashughulikia viongozi wa kijiji wanaoendekeza migogoro kwa kuuza ardhi za malisho za wananchi.

 

Katika hafla hiyo wananchi wa kijiji cha Moita  walimzawadia mkuu huso wa wilaya Ng'ombe baada ya  kutambua mchango wake kwa kurejesha eneo lao la malisho lenye ukubwa wa ekari 10 lililokuwa limeuzwa kinyemela na baadhi ya viongozi wa kijiji hicho.


Katika sherehe hizo viongozi mbalimbali walihudhukua akiwemo mdau wa maendeleo na mafanyabiashara maaruf bilionea Saniniu Laiser















Ends .



Post a Comment

0 Comments