MONDULI :BITEKO AKONGA NYOYO ZA WANA-MONDULI,AAGIZA KUCHUKULIWA HATUA KALI WANAOSABABISHA MIGOGORO YA ARDHI

Na Joseph Ngilisho Arusha 


NAIBU Waziri Mkuu wa Waziri wa Nishati, Dk, Dotto Biteko amesema viongozi mbalimbali watakaobainika kuuza ardhi au kuleta migogoro kwa wananchi watachukuliwa hatua pale itakapobainika.


Aidha amesema serikali itafanya kila namna kuhakikisha wafugaji nchini wakiwemo wa wilaya ya Monduli wanaendelea kuimarika na kuheshimika na kuwa daraja la juu kwa sababu mifugo yao inatathamani na inachangia pato la taifa kwa asilimia saba.


Dk, Biteko aliyasema hayo Wilayani Monduli katika ziara yake wilaya za Arusha kuelekea maadhimisho ya sherehe za miaka 61 ya Muungano wakati akiongea na wananchi shule ya sekondari Migungani One iliyopo wilayani hapo. 


Alisisitiza viongozi wa serikali kazi yao kubwa ni kuhudumia wananchi kwa haki na kuepuka kuuza ardhi za watu na mahali popote na itakapobainika kiongozi kauza ardhi basi sheria ichukue mkondo wake na kusisitiza viongozi kuacha kulumbana badala yake wafanye kazi kwani wananchi wanahitaji maendeleo na si malumbano. 


"Kiongozi atakayebainika kuuza ardhi ya wananchi au kuleta migogoro ya ardhi atachukuliwa hatua na naipongeza wilaya ya Monduli kwa kutatua kero za ardhi na wilaya hii itakuwa ya mfano katika utatuzi wa migogoro ya ardhi"


Alisema katika kuhakikisha wananchi haswa wafugaji mifugo yao inakuwa yenye tija zaidi na kupata maeneo ya malisho na maji serikali imekuwa ikiweka malambo na majosho kwaajili ya mifugo hiyo kupata maji


Alisema serikali inatambua umuhimu wa wafugaji na kuhakikisha wafugaji hao wanakuwa na maendeleo ikiwemo uchumi kukua zaidi


"Mimi ni mfugaji,nimesoma na kulelewa kwa kuuza maziwa na hiyo hii ndiyo biashara ninayoifahamu na Rais Dk,Samia anawapenda wafugaji na ndiyo sababu anahakikisha penye miradi ya maji pia mifugo inapata maji ya kunywa"


Ends.... 



Kuhusu umeme alisisitiza serikali inafanya juhudi kubwa kuhakikisha umeme huo unawafikia wananchi Ikiwemo wananchi wa wilaya ya Ngorongoro kwa kujenga kituo cha kusambaza umeme njia tank pamoja na kituo cha kupoozea ili kuhakikisha nishati hiyo inawafikia pasipo kukatikatika. 

Post a Comment

0 Comments