By Ngilisho Tv
Hati ya mashtka ya Tundu Lissu. Ameshtakiwa kwa kesi mbili zenye mashtaka tofauti.
#KesiYaKwanza ni kutoa taarifa za uongo kinyume na kifungu cha 16 cha sheria no.14 ya makosa ya mtandao. Kesi hiyo ina mashtaka matatu;
1. Kwamba mnamo tar.3 April 2025 katika maeneo ya jiji la Dsm alisema "uchaguzi wa serikali za mitaa, wagombea wa Chadema walienguliwa kwa maelekezo ya Rais"
2. Kwamba mnamo tar.3 April 2025 katika maeneo ya jiji la Dsm alisema "mapolisi wanatumika kuiba kura na vibegi"
3. Kwamba mnamo tar.3 April 2025 katika maeneo ya jiji la Dsm alisema "Majaji ni Ma-CCM hawawezi kutenda haki, wanapenda wapate teuzi na kuchaguliwa kuwa majaji wa mahakama ya rufaa"
#KesiYaPili ni UHAINI kinyume na kifungu cha 39(2)(d) cha sheria ya kanuni ya adhabu. Kwamba mnamo tar.3 April 2025 katika maeneo ya jiji la Dsm alisema "msimamo huu unaashiria uasi, ni kweli. Kwa sababu tumesema tunazuia uchaguzi tunahamasisha uasi. Hiyo ndio namna ya kupata mabadiliko, hivyo tunakwenda kukinukisha"
Kesi ya kwanza yenye mashtaka matatu, amepata dhamana maana kwa mujibu wa sheria kesi ya kutoa taarifa za uongo inadhaminika.
Kesi ya pili ya UHAINI amenyimwa dhamana maana kwa mujibu wa sheria makosa ya aina hiyo hayana dhamana. Hivyo basi amepelekwa gereza la Segerea hadi April 24, 2025 kesi yake itakapotajwa tena.! #FreeTunduLissu #NoReformsNoElection
0 Comments