HABARI YA KUSHTUA,TAZAMA PICHA MTITI WA LISU AKIKAMATWA NA POLISI MBINGA ,ILIKUWA KAMA SINEMA!

 Tundu Lissu Akamatwa na Polisi Mbinga

By Ngilisho Tv 

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma, wilayani Mbinga, mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya Aprili 9, 2025.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, tukio hilo lilitokea mara tu baada ya Lissu kumaliza kuhutubia hadhara hiyo na kuanza kuchangisha fedha kwa wananchi kwa njia ya kampeni maarufu kama “Tone Tone”.

"Baada ya mkutano leo jioni saa 12:00 wilaya ya Mbinga, wakati wa kufunga mkutano OCD alimfuata Tundu Lissu jukwani akamwambia tafadhali ukishuka hapo jukwani ingia kwenye gari ya Polisi nakutaka Polisi kwa mahojiano. Lissu alimwambia nimefanya nini? huku akiendelea kuchangisha fedha katika hadhara 'Tone Tone,'" ameandika Lema kupitia ukurasa wake wa X.

Lema ameongeza kuwa walijaribu kuzungumza na maofisa wa Polisi ili jambo hilo lishughulikiwe kwa utulivu na kwa kufuata taratibu.

"Baada ya kuona hiyo zogo, Kamanda Sosopi alimfuata OCD na kumwambia kama Lissu analo jambo na nyie mnaweza kuja pale tulipofikia mkamchukua kwa utaratibu hapa mtazua tafrani kubwa maana halaiki hapa ni kubwa. Pia mimi nilisisitiza ushauri huo kwa OCD na wasaidizi wake wengine, alionekana kama anaelewa lakini ghafla mabomu ya machozi mengi yalianza kurindima," ameeleza Lema

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, tukio hilo lilitokea mara tu baada ya Lissu kumaliza kuhutubia hadhara hiyo na kuanza kuchangisha fedha kwa wananchi kwa njia ya kampeni maarufu kama “Tone Tone”.

"Baada ya mkutano leo jioni saa 12:00 wilaya ya Mbinga, wakati wa kufunga mkutano OCD alimfuata Tundu Lissu jukwani akamwambia tafadhali ukishuka hapo jukwani ingia kwenye gari ya Polisi nakutaka Polisi kwa mahojiano. Lissu alimwambia nimefanya nini? huku akiendelea kuchangisha fedha katika hadhara 'Tone Tone,'" ameandika Lema kupitia ukurasa wake wa X.

Lema ameongeza kuwa walijaribu kuzungumza na maofisa wa Polisi ili jambo hilo lishughulikiwe kwa utulivu na kwa kufuata taratibu.

"Baada ya kuona hiyo zogo, Kamanda Sosopi alimfuata OCD na kumwambia kama Lissu analo jambo na nyie mnaweza kuja pale tulipofikia mkamchukua kwa utaratibu hapa mtazua tafrani kubwa maana halaiki hapa ni kubwa. Pia mimi nilisisitiza ushauri huo kwa OCD na wasaidizi wake wengine, alionekana kama anaelewa lakini ghafla mabomu ya machozi mengi yalianza kurindima," ameeleza Lema.

Kwa mujibu wa CHADEMA, waliokamatwa pamoja na Lissu ni pamoja na Aden Mayala, Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kusini, Felius Festo, Mratibu wa Uhamasishaji wa BAVICHA Taifa, Shija Shebeshi pamoja na mmoja wa walinzi wa Lissu.

Hadi sasa, Jeshi la Polisi halijatoa taarifa rasmi kueleza sababu za kukamatwa kwa Lissu na wenzake. Tundu Lissu kwa sasa anashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Mbinga

Post a Comment

0 Comments