WAZIRI NDUMBARO ACHARUKA AAGIZA WATUMISHI WA UMMA WALIOSABABISHA MIGOGOROWACHUKULIWE HATUA,AAGIZA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA NGORONGORO ALETWE HARAKA,PADRI AMKAANGA MCHANA KWEUPE!

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 


WAZIRI wa Katiba na Sheria,dkt Damas Ndumbaro ameagiza kuchukuliwa hatua kwa watumishi  wa umma ambao wamekuwa chanzo cha migogoro kwa wananchi ikiwemo ya Ardhi .
Akiongea na umati wa watu wenye Changamoto ya migogoro mbalimbali katika  maadhimisho ya wiki ya  wanawake inayoadhimishwa kitaifa jijini Arusha,Machi 8,2025,waziri alisema Rais Samia amemtuma kwenda Arusha kushughulika na kero za wananchi na alimwagiza kumchukulia hatua mtumishi yoyote wa umma ambaye amekuwa chanzo cha migogoro kwa wananchi 

"Nimekuja kuweka kambi Arusha pamoja na timu ya wanasheria zaidi ya hamsini kutatua migogoro ya wananchi na nikimaliza kuongea na nyinyi naanza kusikiliza kero zenu"

Alisema rais Samia jbSuluhu Hasan amemtuma kuja Arusha kushughulika na
 migogoro ya wananchi na kuipatia ufumbuzi wa kisheria.

"Rais Samia amenituma nije Arusha kuanzia tarehe moja hadi tarehe 8,2025 kushughulika na migogoro ya wananchi,maana yake amedhamiria watu wa Arusha wapate haki zao,nimekuja na timu ya wanasheria zaidi ya 50,tumekuja na wizara ya Ardhi,wizara ya maendeleo ya jamii pamoja na wasaisizi wa sheria ili kutatua kero zenu"

Alisema baadhi ya kero watazimaliza ndani ya siku nane na zile ambazo hazitaisha wanasheria wataendelea nazo kwa gharama ya rais Samia.

Aidha alisema rais Samia ameagiza mtumishi yoyote anayesababisha migogoro achukuwe hatua haraka iwwzekenevyo.

"Ewe mtumishi wa umma ambaye umekuwa chanzo cha kuwadhulumu wananchi wanyonge ,kuwatesa na kuwaonea, arobaini zako zimefika,Samia ameandaa dawa yako imechemka na imeiva nimekuja kukunywesha ili kila mtanzania anapata haki yake"

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kutaka msaada wa kisheria katika mabanda ya katiba na sheria ni pamoja na mkazi wa Ngorongoro Padri Gabriel Ole Kilelo ambaye alimweleza waziri Ndumbaro namna Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ngorongoro na maofisa wa Ardhi walivyo husika kumnyang'anya maeneo yake.

Alisema Mkurugenzi huyo alimnyang'anya Ardhi yake licha ya kutoa bure sehemu ya eneo lake ,kuzuia wafadhili na kumnyima tenda za halmashauri kupitia shirika lake la Kidupo ambalo linashughulika kusaidia watoto wa jamii ya kifugaji ikiwemo kuwasomesha.

Alisema chanzo cha mgogoro wake na halmashauri ya Ngorongoro ni kuitetea serikali katika kutatua mgogoro wa Ardhi  katika eneo la pori tengefu la Loliondo uliodumu kwa miaka 30.

Hata hivyo waziri Ndumbaro aliagiza kuitwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo pamoja na maofisa wa Ardhi wilayani humo kufika katika banda la katiba na sheria kesho February 5,2025.








Ends..










Post a Comment

0 Comments