Na Joseph Ngilisho,ARUSHA
TAASISI ya dini ya Kiislamu ya Twariqa ,Zawiya Kuu Arusha,imempongeza rais Samia Suluhu Hasan kwa Msaada wa sh,milioni 10 kwa ajili ya kufuturisha waislamu hususani makundi maalumu wakiwemo yatima.
Pongezi hizo zimetolewa jana na Naibu katibu Mkuu Twariqa Taifa ,Sheikh Haruna Husein katika hafla ya kufuturisha,iliyofanyika Zawiya Kuu Arusha, ambapo viongozi mbalimbali walihudhulia futari hiyo iliyotolewa na rais Samia.
Mbali na pongezi hizo ,taasisi hiyo iliahidi kuendelea kumuunga mkono rais Samia kwa namna anavyoliongoza Taifa kwa kuendeleza amani iliyoachwa na watangulizi wake ambayo ndio msingi wa Taifa letu.
"Tunamshukuru Rais Samia kwa kutambua mchango wa Taasisi ya Twariqa kwa kuona kwamba Twariqa ni Taasisi inayotambulika na kutupatia zawadi ya kuweza kufuturisha, tunasema mama Asante sana mitano tena!"
Katika hatua Nyingine sheikh aliwaomba waislamu kushikamana na kuwa wamoja hasa kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani na kukemea vikali baadhi ya viongizi wa dini kuendekeza fitina,unafiki na maneno yenye nia ya kuharibu msingi wa dini hiyo.
"Inasikitisha kuona baadhi ya viongozi wa dini kuendekea fitina na majungu mimi kama kiongozi wa dini nimeaminiwa na kupewa wadhifa huu, sipendi kukaa kama mzigo"Alisema Haruna.
Alisisitiza kwa waislamu kurudi katika mafundisho ya dini kwa kuwaheshimu viongozi waliopo madarakani na kuacha kutumia mitandao ya kijamii kulaumu na kuchafuana badala yake washirikiane
Naye mwenyekiti wa taasisi hiyo ya Twariqa sheikh Salim Mubarak pamoja na kumshukuru rais Samia kwa msaada wa fedha za kufuturisha aliwaomba watu wengine wenye uwezo kutumia kipindi hiki cha ramadhani na baada ya ramadhan kusaidia wenye uhitaji.
Aidha aliwataka viongozi wa dini hiyo kutoogopa kusemwa badala yake watumie muda huo kujiimarisha zaidi ili kuleta maendeleo katika taasisi zao za dini.
"Kiongozi lazima ukubaliane kwamba wewe ni jalala na kama unataka kazi nzuri ya kutosemwa nenda kauze Ice cream"Alisema
Kwa upande wake Kiongozi wa msikiti wa Ngarenaro,sheikh Hasan Kileo aliwataka waislamu kujenga utaratibu wa kutii viongozi wao waliopo madarakani,hali itakayoondoa misuguano na migogoro isiyo na tija.
Ends....
0 Comments