By Ngilisho Tv
MWENYEKITI WA Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), Tundu LIssu na Viongozi wa ACT Wazalendo ukiongozwa na Kiongozi wa Chama Dorothy Semu na Mwenyekiti wa Chama hicho, Othman Masoud Othman ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar umezuiwa kuingia nchini Angola na mamlaka za Serikali ya Angola.
Viongozi hao kutoka Tanzania pamoja wengine kutoka nchi mbalimbali wamezuiliwa katika Uwanja wa Ndege wa Luanda na hati zao za kusafiria nazo zinadaiwa kushikiliwa pia.
Serikali ya Angola, bila kueleza sababu yoyote imetoa amri ya viongozi hao kurejeshwa Tanzania.
Viongozi hao wa siasa kutoka Tanzania waliwasili Angola kushiriki mazungumzo ya Jukwaa la Demokrasia Afrika (The Platform for African Democrats (PAD)] yaliyoandaliwa na Taasisi ya The Brenthurst Foundation yaliyopangwa kufanyika kuanzia Machi 13-16 mwaka huu.
Mbali na Lissu na viongozi wa ACT Wazalendo, viongozi wengine zaidi ya 40 kutoka nchi mbalimbali Afrika ambao pia walikuwa wanahudhuria mkutano huo wamezuiliwa na serikali ya nchi hiyo huku sababu ya kufanya hivo ikiwa bado haijaelezwa.
Moja ya viongozi waandamizi waliotarajiwa kushiriki kwenye Mkutano huo ni pamoja na Marais Wastaafu Ian Khama (Botswana) na Andres Pastrana Arango (Columbia).
Wengine ni Waziri wa Kilimo wa Afrika ya Kusini na Kiongozi wa Chama cha DA, John Steenhuisen na Kiongozi wa Chama cha PODEMOS cha nchini MsumbijiNdugu Venancio Mondlane.
0 Comments