Na Joseph Ngilisho-ARUSHA
WATUMISHI Wanawake wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) wameungana na maelfu ya wanawake kutoka sekta mbalimbali kushiriki katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Kitaifa jijini Arusha.
Maadhimisho hayo, yenye kaulimbiu "Wanawake na Wasichana 2025, Tuimarishe Haki, Usawa na Uwajibikaji" yamefanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha huku Mgeni rasmi akiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
EWURA imetumia maadhimisho hayo kuonesha na kuhimiza ushiriki wa wanawake katika sekta ya matumizi sahihi ya nishati safi na Salama kupitia Banda la maonesho lililokuwa katika maeneo ya uwanja huo.
Katika banda hilo Wanawake hao wametoa elimu ya uelewa na kuhamasisha uwekezaji wa gesi asili ya kupikia (LPG), matumizi ya nishati safi ikiwa ni hatua ya kuunga mkono kampeni ya serikali ya kuhakikisha teknolojia ya matumizi ya nishati inaenea pote Nchini.
Maonesho hayo ambayo yamefana sana ,Ewura imekuwa na kipaumbele cha wanawake na nishati safi ya kupikia na inasimamia UMEME,PETROL,GESI ASILI NA USAFI WA MAZINGIRA.
ENDS...
0 Comments