RC MAKONDA AWAANGUKIA WABUNGE MAENDELEO YA MKOA WA ARUSHA!

By Ngilisho Tv -ARUSHA

MKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amewaomba wabunge wa Bunge la Tanzania kuunga mkono agenda mbalimbali za maendeleo yanayotakiwa kufanyika mkoani Arusha ili kuupaisha mkoa huo kiuchumi.


Makonda ameyasema hayo leo Machi 14,2025 wakati akiongea na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii huku akiwaomba wabunge wanaounda kamati hiyo kuunga mkono ajenda mbalimbali za maendeleo zinazowasilishwa bungeni


Katika mazungumzo yao RC Makonda amezungumzia miongoni mwa ajenda tarajiwa zinazohusu Mkoa wa Arusha ni pamoja na mpango wa Rais Samia Suluhu Hassan wa kujenga Reli ya Kisasa (SGR) itakayotoka Tanga kwenda Arusha kuungana na mpango mwingine wa serikali wa ujenzi wa bandari kavu mkoani Arusha itakayounganishwa na Bandari ya Tanga kwa ajili ya kuhudumia nchi za DR Congo, Burundi, Uganda na Rwanda.


Kulingana na Makonda, Bandari ya Tanga kwa sasa ni ya pili kwa kupokea shehena nyingi zaidi za mizigo nchini, ikitokana na uwekezaji wa takribani bilioni 500 zilizowekezwa na serikali, suala ambalo limesababisha barabara za Arusha kuwa na msururu mrefu wa malori kutoka 60 ya awali hadi kufikia malori 600 kwa siku yanayoelekea nchi za nje na hivyo kujengwa kwa reli hiyo ya kisasa kunatajwa kuwa kutarahisisha huduma za usafiri na usafirishaji wa shehena za mizigo

Post a Comment

0 Comments