RAIS SAMIA AMWAGA MAPESA ZAWIA KUU ARUSHA,ZITATUMIKA KUFUTULISHA FUTARI, SALIMU MWALIMU AKIBIDHI TAZAMA MAPICHA!

 Na Joseph Ngilisho -ARUSHA 


RAIS Samia Suluhu Hasani ametoa msaada wa futari kwa waumini wa taasisi ya dini ya kiislamu ya Twariqa mkoani Arusha kwa ajili ya kufuturu katika kipindi hiki cha mfungo wa ramadhani.


Msaada huo ambao ni fedha umekabidhiwa leo Machi 12,2025 katika Zawiya kuu jiji Arusha na Salim Mwalimu kutoka Zanzibar ambaye alimwakilisha Rais Samia  katika hafla fupi iliyoambatana na kuzuru kaburi la Kiongozi wa taasisi ya Twariqa , Zawiya kuu,Marehemu Daruweshi Mti Mkavu.

Salimu aliwasihi  waumini wa dini hiyo kuendelea kujitoa kwa ajili ya wengine wakati huu wa mfungo Mtukufu wa Ramadhani na hata baada ya mfungo. 

Amewaasa waumini hao kutenda mema kama ambavyo mwezi Mtukufu wa Ramadhani unavyofunza pamoja na9 kuendelea kuchangia katika masuala muhimu kwaajili ya Mwenyezi Mungu ikiwemo katika nyumba za ibada.

"Nilipokea ombi la msaada wa futari kutoka kwa Sheikh haruna kuhusu hitaji la kufuturisha waumini wasio na uwezo  na mimi kama mwislamu niliguswa na kuamua kuliwasilishwa suala hilo kwa Mama ambaye aliguswa na kuniomba kuwakilisha msaada huo kwa niaba yake"

Aidha Mwalim aliguswa na  mahitaji ya msikiti huo wa Zawia Kuu ambapo vijana wanaosoma dini na kuishi katika msikitini huo ,wanalala katika mazingira magumu na kuhitaji msaada zaidi wa malazi pamoja na ukarabati wa msikiti huo.


Alisema Taasisi ya Twariqa ni taasisi kongwe ya dini ya kiislamu kuingia hapa nchini hivyo kitendo cha Rais samia kutoa futari ni jambo jema kwani linaakisi uhalisia na wanatarajia kufuturisha makundi mbali.

"Tunamshukuru sana Rais Samua kwa kuikumbuka Zawia kuu kwa kutupatia msaada wa fedha amvazo zitatumika kuandaa futari kwa ajili ya makundi maalumu wakiwemk yatima"Alisema Haruna ambaye pia ni naibu katibu Mkuu Twariqa

Aliwataka wanasiasa kumuunga mkono rais Samia kutokana na moyo wake wa kutoa msaada bila kubagua.













Ends...



Post a Comment

0 Comments