PAC YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI MIKUBWA YA KIKULETWA YA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA.

 Na Joseph Ngilisho- HAI

KAMATI ya Kudumu ya bunge ya hesabu za serikali (PAC),imeridhishwa na utekelezaji wa mradi mkubwa wa kimkakati wa chuo cha ufundi (ATC) Arusha,wenye lengo la kuboresha Elimu ya ufundi katika ukanda wa afrika Mashariki  (EASTRIP ) katika wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro.

Mradi mwingine unaotekelezwa ni ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu ya maji  Hydropower Project (KIHPP), wenye thamani ya dola za kimarekani sh,milioni 4.6 sawa na sh,bilioni 11.8 za kitanzania.


Akiongea mara baada ya kamati hiyo kutembelea miradi hiyo Makamu Mwenyekiti wa  PAC, Japhet Hasunga pamoja na wajumbe wa kamati hiyo walidai kuridhishwa na  hatua iliyofikiwa ya miradi hiyo hasa baada ya kujionea uhalisia wa ujenzi wa kituo cha kufua umeme sanjari na majengo mbalimbali yaliyojengwa na serikali kupitia Mradi wa Ushirikiano wa Kikanda wa Afrika Mashariku(EASTRIP) nankueleza kwamba chuo hicho kimepiga hatua kubwa.



Hasunga amepongeza juhudi za serikali katika kuhakikisha kampasi hiyo inakuwa mahiri katika ufundishaji wanafunzi kwa vitendo na kuagiza samani pamoja na mahitaji mengine muhimu yawepo ili wa mafunzo hao w watakapoanza masomo kwenye kampasi hiyo wasikumbane na changamoto za vifaa vya kujifunzia ikiwemo samani


“ATC mnahitaji pongezi kwanza  ni kwa mradi huu wa umeme lakini pia majengo yenu ni ya kisasa hapa Rais Samia Suluhu Hassan  ametekeleza sera ya elimu kwa vitendo zaidi, thamani ya fedha inaonekana”


Akizungumzia kuhusu mradi huo Mhandisi msimamizi wa Mkandarasi , Emmanuel Norberts kutoka kampuni ya kichina ya HNAC Technology Co Ltd ambao ndio wanatekeleza mradi huo kwa kushirikiana na kampuni ya wazawa ya Whitecity International Contractors Ltd amesema kuwa mradi huo wa kufua umee umefikia asilimia 20 kwa sasa .

Emmanuel alisema kuwa, mitambo inayotegemewa kutoka nje ipo tayari kwa asilimia 95 ambapo amesema mradi huo utatumika kama kiwanda cha kufundishia wanafunzi wa chuo cha ufundi kwa vitendo hususani wanaosomea maswala ya umeme.

Alisema kuwa ,mradi huo utazalisha  megawati 1.65 ambapo umeme mwingine utaingizwa  kwenye gridi ya Taifa  kwani watauzia Tanesco .

“Mradi huu ulianza rasmi may 14  mwaka jana ambapo unatarajiwa kukamilika.rasmi oktoba 13 ,2025 ambapo umeweza kutoa ajira kwa vijana wazawa 57 kutoka vijiji vya karibu na mradi huu.”alisema Emmanuel. 


Naye Mhandisi mshauri wa mradi huo, dkt Robert Kabudi  alisema mradi huo ulianza Mei 13,2024 na unatarajia kukamilika Oktoba 13 ,2025 na kwa sasa mradi huo unaendelea huku wakisubiri mitambo inayotengenezwa nje ya nchi ifike nchini lakini ukikamilka utasaidia vijiji vya jirani ikiwemo kutumika kama kitui cha kufundishia wanafunzi kwa vitendo jinsi ya kuzalisha umeme na kinatarajia kutoa megawati 1.65 .

Alisema mradi huo wa mtambo wa kufua umeme unafanyika kwa awamu tatu na kwa sasa upo katika utekelezaji wa awamu ya kwanza na umefikia asilimia 20  wenye thamani ya zaidi ya Sh  bilioni 9.930 ambao ukikamilka utasaidia wanafunzi wanaosoma kampasi hiyo kufanya kazi kwa vitendo.

Loop

Wakati huo huo, Mkuu wa Chuo cha ATC, dkt Musa Chacha alisema  chuo hicho kilipokea kiasi cha sh, bilioni 37.657 kwaajili ya ujenzi wa majengo 11 katika kampasi ya Kikuletwa ikiwemo hosteli, bwalo la chakula na nyumba za maunganisho ya umeme, jengo moja lenye madarasa matano ikiwemo ukumbi wa mihadhara na karakana tatu


Baadhi ya wabunge wa kamati hiyo, Esther Matiko mbunge wa viti maalum Mkoa wa Mara na Emmanuel ole Shangai kutoka Jimbo la Ngorongoro wamepongeza serikali kwa kutoa fedha kwaajili ya chuo hicho ikiwemo uzalishaji wa umeme wenye tija zaidi kwa nchi.





 


Ends...

Post a Comment

0 Comments