NEMC YAKABIDHI MAJIKO MANNE YA GESI YENYE THAMANI YA SH,MILIONI 10 KWA SHULE YA MSINGI YA ARUSHA, SHULE HIYO INA MIAKA 80 HAIJAWAHI KUTUMIA GESI ,NI KUNI NA MKAA KWA KWENDA MBELE!

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

 

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)limetoa masaada wa Majiko Manne ya kupikia Yenye thamani ya sh, Milioni 10 kwa shule ya Msingi Arusha (Arusha Day)katika maadhimisho ya siku ya mwananke duniani,ambayo kitaifa yamefanyika jijini Arusha.

Akikabidhi Majiko hayo mwakilishi wa Mkurugenzi wa NEMC,Lilian Lukambuzi, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tathmini ya mazingira kwa jamii (NEMC), alisema wameamua kutoa majiko hayo ikiwa ni mpango wao wa kuunga mkono mkakati wa serikali wa kuhamasisha matumizi sahihi ya nishati safi na salama ya kupikia.

"Tukio hili la kukabidhi Majiko haya ni kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia na katika kutekeleza maono ya Rais Samia ,ambapo serikali ilikuja na mpango wa miaka 10 uliozinduliwa mwaka 2024 unaotarajiwa kukamilika mwaka 2034"

"Mkakati huo wa serikali lengo lake ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2034 asilimia 80 ya watanzania wawe wamehamia kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikia na kuachana na matumizi duni ya kuni "

Alisema miongoni mwa mkakati wa serikali ni pamoja na kuzitaka taasisi ambazo bado zinapikia  watu zaidi ya mia moja kuachana na matumizi ya nishati chafu za kupikia ambazo zinaathiri kubwa kwa  watoto na wanawake.

Alisema katika kutekeleza mkakati huo wa serikali NEMC imeamua kutoa msaada huo wa majiko manne pamoja na miundo mbinu yake ya kutumia gesi yakiwa na thamani ya sh,milioni 10 na kati ya hayo majiko matatu yanachukua wastani wa  lita 200 na jiko moja, lita 100.

"Majiko haya wakiyatumia vizuri yatasaidia kulinda Mazingira,afya kwa jamii na kuboresha maisha na kurahisisha majukumu ya mpishi "

Awali mwalimu mkuu wa shule hiyo Hashimu Njau alisema tangu kuanzishwa kwa shule hiyo miaka 80 iliyopita wamekuwa wakitumia kuni na mkaa jambo ambalo limechangia uharibufu wa mazingira na  kuathiri afya za wanafunzi na wapishi.

Mwalimu Njau aliishukuru NEMC kwa msaada huo ambao alidai utabadilisha mazingira ya shule hiyo  yenye jumla ya wanafunzi 1600 na kuzitaka taasisi zingine kuiga mfano huo ili kutokomeza matumizi yasiofaa ya kuni na mkaa .









Ends...








Post a Comment

0 Comments