By Ngilisho Tv
Msanii Joyce Mbaga maarufu kama Nicole Berry amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam kwa ajili ya kujibu mashtaka ya tuhuma zinazomkabili.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Muliro Jumanne alithibitisha kumshikilia Nicole mnamo Machi 3, 2025 kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo za kukusanya fedha kupitia WhatsApp bila kibali na kisha kuzima simu yake.
Kauli ya Jeshi la Polisi ilifuatiwa na malalamiko kutoka kwa Watu mbalimbali wakidai kucheza upatu kwa Nicole lakini hakuwapokelea simu walipotaka kuwasiliana nae.
0 Comments