By Ngilisho Tv
Mwanamke mmoja ambaye jina lake halijafahamika amekutwa akiwa mtupu katika ofisi za Shirika la umeme nchini (TANESCO) Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.
Kamanda wa Polisi Mkoani humo Marco Chilya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo saa tisa usiku wa kuamkia Machi 11, 2025 ambapo ameeleza kuwa mara baada ya mwanamke huyo kukutwa kwenye jengo la ofisi za Tanesco
Mwanamke huyo inadaiwa alikuwa akisafiri kwa ungo kutoka Mkoani Mtwara akielekea Nyasa lakini hakufanikiwa na kuishia kuanguka kwenye ofisi hizo.
Maafisa wa Polisi wamempeleka mwanamke huyo kwenye Hospitali ya Mkoa wa Songea (HOMSO) kwa uchunguzi zaidi ili kubaini afya yake ikiwemo kama ana tatizo la akili.
Credit; EastAfricaTV
0 Comments