MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema.
By ngilishonews.com
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema.
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema, amesema hatogombania Ubunge katika Jimbo la Arusha kama hakutafanyika mabadiliko ya sheria za mfumo wa uchaguzi.
Lema, amejitenga kwa muda na viongozi wakuu wa CHADEMA kwa sasa, walioanza Kampeni ya siku 48 za ‘No Reform No Election’ kwa kufanya mikutano ya nchi nzima.
Lema, amepanga kuzungumza na wakazi wa Jiji la Arusha, Alhamisi ya Machi 27 mwaka huu katika viunga vya Soko Kuu.
Akizungumza na Nipashe Digital leo, Machi 25, 2025, amesema moja ya ajenda zake katika mkutano huo, ni kuwaeleza wakazi wa Arusha kuhusu msimamo wa chama hicho, kupitia kampeni yao ya 'no reforms, no election'.
“Hii ajenda ya 'no reforms, no election' ni muhimu kwa nchi nzima na sio kwa chama chetu pekee. Sitagombea Ubunge kama hakutakuwepo na reforms katika sheria na kanuni za uchaguzi.…Hata kama nitaambiwa Jimbo hili nitapewa, mimi sitaki zawadi ya jimbo hilo, kwangu itakuwa mkosi.”
Ajenda nyingine, ni kukemea kauli iliyotolewa na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) nchini, Amos Makalla, ambayo imeibua mjadala mzito, baada ya kutoa tuhuma nzito kwa CHADEMA.
0 Comments