Na Joseph Ngilisho ARUSHA
HALMASHAURI ya Jiji la Arusha imeingia lawamani kufuatia kitendo chake cha kuvamia na kuvunja uzio ,uliozungushiwa kwa ajili ya kukarabati kituo cha Mafuta katika eneo la Soko kuu mali ya Mfanyabiashara Tom Masuki bila kufuata utaratibu na kusababisha hasara kubwa.
Tukio hilo limetokea majira ya asubuhi ya February 28,2025 baada ya mwanasheria wa jiji Iddy Ndahona kuongoza genge la migambo wa jiji zaidi ya ishirini kuvunja uzio huo na kusababisha uharibifu wa mali wakati wanakibali halali cha ukarabati toka jiji .
Akizungumza tukio hilo mfanyabiashara Thom Masuki amelalamikia tukio hilo akidai kwamba kitendo kilichofanywa na jiji ni uonevu mkubwa kwa sababu amefuata taratibu zote na kupata vibali kwa ajili ya kukarabati eneo lake la kituo cha mafuta ila ameshangaa siku moja mara baada ya kuzungumzia uzio jiji wamekuja kuvunja.
Alidai kuwa jiji wanadai kwamba uzio uliojengwa upo eneo la watembea kwa miguu, jambo ambalo si kweli kwani eneo la watembea kwa miguu lipo kwenye Lami na wao hawakufikisha nguzo za uzio kwenye Lami na tunavibali vyote vya ukarabati"
"Hapa kinachoendelea ni diwani Tojo wa kata ya kati kutuhujumu kwa sababu tumepata taarifa kuwa kuna Wafanyabiashara anataka kuwapatia wazungushie maduka hatutakubali"
Aidha mfanyabiashara huo amemwomba mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda kumsaidia kwa kuwa jambo hilo amebaini kuwepo kwa viongozi wenye nia ovu ya kuleta mgogoro kwa maslahi yao binafsi.
Naye meneja wa mfanyabiashara huyo, Raphael Eliya Mollel alisema kuwa jana majira ya jioni walizungushia uzio wa mabati ili kuanza ukarabati wa kituo hicho cha mafuta baada ya kusimama kwa muda mrefu lakini majira ya asubuhi walikuja migambo wa jiji na kuvunja uzio huo bila kueleza sababu za msingi.
Aidha meneja huyo alidai kuwa upo mpango wa maksudi unaolenga kuwapa Wafanyabiashara wengine kujenga maduka katika eneo hilo unaodaiwa kuratibiwa na diwani Abdul Tojo wa kata ya kati jambo ambalo kimsingi linaweza kusababisha mgogoro usio natija katika eneo hilo ambalo ni mali ya Mwekezaji Masuki.
Akihojiwa kwa njia ya simu mwanasheria wa jiji Iddy Ndabhona alisema walipata taarifa kuwa uzio huo kujengwa kwenye njia ya watembea kwa miguu ndipo walipofika na kuamua kuvunja.na alipohojiwa kwanini hawakuweka alama ya x ikimaanisha ondoa na wao kuamua kuvunja kibabe, alisema walikaidi kuvunja kwa hiari ndio maana walitumia nguvu ya migambo .
Naye diwani wa kata ya kati ya Abul Tojo alidai kuwa mfanyabiashara huyo amezungushia uzio usiku bila kufuata utaratibu na hakuwa na kibali .
Ends..
0 Comments