DC MKUDE AKUNJUA MAKUCHA ATAKA JENGO LA HOSPITALI YA WILAYA ARUSHA LA BILIONI 17,KUKAMILIKA KWA WAKATI UJENZI UWE USIKU NA MCHANA ,AAGIZA MILANGO ISIYO NA UBORA KUNG'OLEWA HARAKA!


 Na Joseph Ngilisho,ARUSHA

Mkuu wa wilaya ya Arusha,Joseph Mkude ameagiza ujenzi wa mradi wa jengo la hospitali ya wilaya  lenye hadhi ya kimataifa linalojengwa kwa thamani ya sh,bilioni 17 katika kata ya Engutoto ,jijini hapa kufanyakazi usiku na mchana ili ifikapo Mei mwaka huu mradi huo uwe umekamilika .

Mkude DC Arusha!

Akiongea wakati alipotembelea mradi huo pamoja na jengo la utawala la halmashauri ya jiji la Arusha,akiwa na kamati ya ulinzi na usalama,Mkude alieleza kurishishwa nabmtekelezaji wa miradi hiyo ila aliagiza  mamlaka zinazosimamia jengo la hospitali kuhakikisha linajengwa kwa ubora unaotakiwa na kukamilika kwa wakati.


Alisema hospitali hiyo ni muhimu sana katika jiji la Arusha kwani mbali na kutoa huduma kwa wazawa ,itatoa huduma kwa watalii na jengo hilo litakuwa na uwezo wa kutua kwa helkopita .

"Jengo hili lipo katika hatua nzuri ya kukamilika kwa awamu ya kwanza ,ninachosisitiza lijengwe usiku na mchana na kwa ubora ili ikamilike na kuanza kutoa huduma mara moja"


Hata hivyo mkuu huyo wa wilaya alikerwa na kiwango hafifu cha miundo mbinu ya milango iliyowekwa katika jengo hilo na kuagiza iondolewe haraka.


"Jengo hili linajengwa kwa gorofa tatu na linajengwa kwa awamu tofauti na awamu ya kwanza tumetenga sh,bilioni 4.2 "


Akizungumzia mradi wa jengo la utawala la jiji la Arusha ,mkuu huyo wa wilaya alimwagiza mkandarasi kuhakikisha ifikapo Mei mwaka huu mradi wa jengo hilo uwe umekamika.


Diwani wa kata ya Engutoto Karimu Moshi alimpongeza rais Samia suluhu Hasan kwa kuwapatia fedha nyingi ikiwa bi mapatonya ndani kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo ya wilaya itakayokuwa na uwezo wa kuhudumia wagonjwa wengi.


Alisema hopitali hiyo itakuwa mkombozi kwa wakazi wa Engutoto pindi itakapokamilika kwani itawaleza kuondoa changamoto ya huduma ya afya kutokana na huduma za kisasa zitakazokuwa zikitolewa.


Enda. 






Post a Comment

0 Comments