Na Joseph Ngilisho- ARUSHA
MADIWANI wa halmashauri ya jiji la Arusha ,wamegoma kugawa mara mbili kwa jimbo la Arusha mjini wakidai ukubwa uliopo sasa unakidhi mahitaji ya wananchi.
Aidha madiwani hao wakubali kugawanywa kwa kata nane za jiji hilo ili kuwasogezea karibu mahitaji ya wananchi ambao wamekuwa wakipata shida ya kukidhi Changamoto zao.
Akiongea katika baraza Maalumu la madiwani meya wa jiji hilo Maximilian Iranghe alisema kuwa madiwani wa kata 25 za jiji hilo pamoja na viti maalumu kwa pamoja wamekataa kugawanywa kwa jimbo hilo na baadhi yao walidai lilikuwa ni shinikizo la wanasiasa kujinufaisha.
Kutogawanywa kwa jimbo hilo huenda ikawa ni dariri mbaya kwa wanasiasa waliokuwa wakipiga kampeni usiku na mchana ili kugawanywa mara mbili kwa jimbo hilo kwa maslahi yao .Alisema Diwani katika mahojiano maalumu.
"Kikao cha leo lilikuwa ni baraza Maalumu la Madiwani likiwa na ajenda moja ya kufanya mchakato wa kugawa jimbo la Arusha ila kwa pamoja baraza limeadhimia kutogawanywa kwa jimbo hilo ila kata nane zenye ukubwa ndizo zitagawanywa "
Meya alisema kuwa mpango huo wa kugawa jimbo hilo la Arusha mjini kwa sasa haupo kutokana na kutokidhi idadi ya watu ambao ndio kigezo pekee cha kugawa jimbo.
"Baada ya vuta ni kuvute madiwani wote wameridhia kutogawanywa kwa jimbo la Arusha mjini kwa sanabu ni dogo lina ukubwa wa kilometa za mraba 272 na wakati tulikuwa tunatafuta hadhi ya jiji tulikuwa na kilometa za mraba 93 ikabidhi tuongezwe na kufikia Kilometa 272"
Alisema kuwa madiwani hao wameridhia kugawanywa kwa kata nane ambazo ni kata ya Muriet,Moshono,Sokoni1,Sinoni, Lemara na Terath.Miongoni mwa kata hizo zitagawanywa mara tatu na kufikia jumla ya kata 35 zitakazounda jiji la Arusha.
"Mchakato wa kugawa majimbo ni maelekezo kutoka tume ya uchaguzi ili kuweza kuboresha shughuli za maendeleo na sio mashinikizo ya wanasiasa"Alisema Meya.
Naye diwani wa kata ya Sakina Vicent Willson alisema kuwa wao kama madiwani hawakuona haja ya kugawa jimbo la Arusha mjini kwa sababu bado linahimilika kuwa na mwakilishi mmoja.
Alisema suala la kugawanywa kwa kata walipokea mapendekezo kutoka kwa baadhi ya madiwani wa kata hizo baada ya kufanya mchakato kutoka kwenye vikao vya Kamati ya Maendeleo ya Kata (Ward Development Committee -WDC) na wao wamebariki mchakato huo .
Ends..
0 Comments