Na Joseph Ngilisho ARUSHA
KESI ya Kupinga Msimamizi wa Mirathi namba 22575 ya mwaka 2024 iliyofunguliwa na ndugu wa Marehemu Taitas Aron Mollel aliyefariki mwaka 1998 imechukua sura mpya baada ya mmoja ya walalamikaji kujitoa katika shauri hilo akiieleza mahakama kwamba alirubuniwa kwa kupewa sh,500,000 ili kufungua shauri hilo.
Mbele ya Jaji Nyigulila Mwaseba wa Mahakama kuu kanda ya Arusha,mlalamikaji, Ester Titus Aron aliileza mahakama hiyo kwamba hawezi kuendelea na shauri hilo , kwani roho yake inamuuma kuona akiisaliti familia yake .
Mlalamikaji huyo alisema aliletewa makaratasi na kusaini kitu asichokijua kwa kuwa yeye hajui kusoma na kuandika na baadaye alijulishwa kwamba ni kwa ajili ya kufungua kesi ya kuwapinga wasimamizi wa mirathi ,William Titus Aron Mollel (Baraka) na Peter Temu.
Mlalamikaji mwingine katika shauri hilo ni Mzee wa ukoo Rorian Meishekini ambaye aligoma shauri hilo kuondolewa mahakamani akidai maamuzi ya mwenzake hakubaliano nayo na yeye anachotaka kesi hiyo iendelee hapa hapa mahakamani ili haki itendeke.
"Ninachotaka kesi iendelee hapa hapa mahakamani tumechoka na vurugu kule nyumbani hakuna maelewano"Alisema Mlalamikaji.
Baada ya Maelezo hayo Jaji Mwaseba aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 6,mwaka huu itakapo kuja kwa ajili ya Kutajwa .
Wakili wa utetezi ,Vincent Bwana kutoka kampuni ya uwakili ya Law Access alisema kuwa shauri hilo lilikuja kwa mara ya tano kwa ajili ya kutajwa baada ya kufunguliwa oktoba Mwaka jana 2024 na walalamikaji wawili akiwemo mzee wa ukoo na mtoto wa marehemu wakiwapinga ndugu zao ambao ni wasimamizi wa mirathi.
"Leo kilichotokea mahakamani ni mlalamikaji mmoja kati ya wawili waliofungua shauri hilo la kumpiga msimamizi wa mirathi kuamua kujitoa akiwa na maana kwamba hana nia ya kuwashtaki ndugu zake na alifungua shauri hilo baada ya kurubuniwa na mtu mmoja aliye mtaja kwa jina la Philemon Mollel (Monaban)"
Akiongea nje ya Mahakama Mshtakiwa William Titus Aron Mollel alimtupia lawama mfanyabiashara Philemon Mollel (Monaban) kwamba anaingilia familia yao kwa kuwarubuni ndugu zake wafungue kesi ya kuwakataa wasimamizi wa mirathi waliochaguliwa kwa mujibu wa sheria.
Hata hivyo ndani ya Mahakama mbele ya jaji Mwaseba, William alihoji uhalali wa Monaban kuwepo mahakamani hapo wakati sio ndugu wa familia hiyo .
William alidai kuwa Monaban anania ovu ya kuivuruga familia yao kwa maslahi yake huku akienda mbali kwa kudai kwamba anataka mgawo wa mali za marehemu baba yake kinyume cha utaratibu na hii ni kutokana na kwamba Monaban anachuki binafsi baada ya William kumshinda katika kesi ya kugombea eneo la familia hiyo alilokuwa amevamia kinyume na utaratibu.
"Kiongozi mkubwa kama Monaban ambaye ni Askofu wa Kanisa la Kilutheli Afrika Mashariki (KKAM) kuingilia mambo ya familia yetu na kuratibu kesi kwa ajili ya kuwaondoa wasimamizi wa mirathi kwa kuwakusanya ndugu zangu kuja kidai mirathi, kwa kifupi Monaban anataka mgawo wa mali za marehemu,Monaban sio ndugu yetu na wala hatuna mahusiano yoyote ya kiukoo na nia ovu ya kutufarakanisha "Alisema William.
Aidha William alihoji kwa kusisitiza kuwa inakuwaje Kiongozi mkuu wa Kanisa Kama Askofu Monaban kuendelea kuifuata fuata Familia ya marehemu Titus kwa kurubuni ndugu kwa kutoa fedha kwa lengo la kuwagawa.
William alimtaka Kiongozi huyo kujitafakari iwapo anafaa kuendelea na wadhifa huo wa kichungaji.
Ends.
0 Comments