WIZARA YAZINDUA KAMPENI YA STAPELIKI LENGO NI KUWABANA MATAPELI WA MITANDAONI

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imezindua kampeni ya” Sitapeliki ” yenye lengo la kuhakikisha wananchi hawatapeliwi na matapeli bali watawasiliana na kampuni za watoa huduma kupitia namba 100 pekee.


Aidha serikali imeanza maandalizi ya ujenzi na ukarabati wa vituo vinane vya ubunifu katika mikoa minane ili kuboresha mazingira ya watafiti na wabunifu wa Tehama  nchini.

Hayo yameelezwa mapema  leo  February 20,2025 jijini Arusha na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha serikali na wadau wa sekta ya mawasiliano na teknolojia ya Habari kuhusu utekelezaji wa mkakati wa taifa wa uchumi wa kidigitali 2024/25

Silaa ametaja mikoa hiyo kuwa ni  Dar es Salaam, Dodoma, Arusha, Mbeya, Tanga, Lindi, Zanzibar na Mwanza lakini pia vituo  hivyo pia vitawezesha ujenzi wa vyuo viwili vya umahiri vya Tehama ambayo vinajengwa Dodoma eneo la (Nala) na Kigoma (Buhigwe)  huku taratibu za ujenzi  zikiendelea.




Alisema vyuo hivyo ni  mahususi kwa utoaji wa ujuzi kwa vitendo hivyo mitaala yake itakuwa ya kumuwezesha mwananchi kupata ujuzi na kuweza kujiajiri vijana


Alisema katika kuelekea uchumi wa kidigitali serikali kupitia wizara hiyo imeratibu ujenzi wa mfumo wa kitaifa wa kuunganisha mifumo yote ya Tehama nchini ijulikanayo kama “Jamii X-Change” .


Alisema jumla ya mifumo 898 imeunganishwa katika miundombinu 14 ya kubadilisha taarifa ambapo  mifumo 514 ni ya serikali huku mifumo 384 ni ya sekta binafsi lakini pia mifumo ya jamii namba na jamii malipo imetengenezwa kwa ajili utambuzi na huduma za malipo “cashless”



Ends....

Post a Comment

0 Comments