By Ngilisho Tv
Mwalimu wa Shule ya Msingi Itete kata ya Kirando Wilayani Nkasi, Clarence Mwanakurya (29) amekamatwa na Polisi kwa tuhuma za kumuoa Mwanafunzi wa kidato cha kwanza Jesca Mwanji (20) tangu mwaka jana na kuishi naye katika majengo ya Serikali yaliyopo katika Shule ya Msingi Itete anaposoma Mwanafunzi huyo.
Haya yamebainika baada ya Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Peter Lijuakali kuanza oparesheni ya kuzuia na kupambana na mimba za utotoni ambapo amewataka Walimu wa Msingi na Sekondari kuziheshimu sketi za shule kwani zitawaletea matatizo katika kazi zao na maisha kwa ujumla, oparesheni hiyo imeanza tarehe 01.11.2021 itaendelea mpaka wabainike waliowaachisha Shule Wanafunzi na kuwaoa.
Kwenye picha wa kwanza kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo akiwa amefungwa pingu pamoja na Clarence, sababu ya Mwalimu Mkuu kukamatwa ni kukaa kwake kimya na kuruhusu Clarence kuishi kuishi na Mwanafunzi huyo.
Ends..
0 Comments