TLP YAPINGA UCHAGUZI WANACHAMA WACHACHAA WADAI WAHUNI WALIOKOTWA VICHOCHORONI , MSAJILI ATOA SIKU SABA AKITAKA MAELEZO!

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 


MSAJILI wa Vyama vya Siasa Nchini,ameupa  muda wa siku Saba Uongozi wa Chama cha Tanzania Labour Part  (TLP), kutoa ufafanuzi wa madai ya ukiukwaji wa Katiba ,Kanuni za Chama hicho kikongwe cha Siasa Nchini kufuatia malalamiko yaliyowasilishwa ofisini kwake na Wanachama wa Chama hicho Nchini.


Katibu Mwenezi wa TLP,Taifa ,Jofrey Stivini,amewaambia wanahabari Jijini Arusha kwenye hoteli ya Equter, kwamba wanachama wa Chama hicho wamemwandikia barua Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini ya kupinga uchaguzi 

uliofanyika February 2 mwaka huu kwenye hoteli ya Mrina iliyopo Manzese Jijini Dar es Salaam ,wakidai kwamba Uongozi wa Taifa uliopo madarakani haupo kihalali.


Amesema kwenye barua yao Wanachama wanapinga Uongozi huo kwa sababu  Viongozi wa Taifa walipo hawakuchaguliwa na Wanachama halali bali wamechaguliwa na watu wa kuokoteza mitaani waliovalishwa sare za Chama hicho.


Jofrey,amesema kuwa Chama hicho kina Wanachama mikoa yote Bara na Visiwani ambapo Jumla ya wajumbe ni 185 na walioshiriki kwenye uchaguzi uliofanyika uliowaweka Viongozi waliopo madarakani Viongozi hao hawakuchaguliwa na Wanachama halali waliopo kwenye Rejesta ya Wanachama.


Amesema kutokana na ukiukwaji wa Katiba ya Chama hicho Wanachama walilifikisha swala hilo kwa Msajili,ambae ametoa muda wa siku Saba kwa Uongozi huo  uliopo madarakani .


Amesema kuwa taarifa ya Mkutano mkuu ilitolewa ndani ya muda wa siku mbili ambao ni kinyume na katiba na kanuni za uchaguzi za Chama hicho hivyo kusababisha wajumbe wa Mkutano mkuu wa mikoa iliyoko mbali kushindwa kuhudhuria na badala hivyo uchaguzi huo ni batili.


Amesema mkutano mkuu uliitishwa kwa ujanja ujanja na aliekuwa Katibu mkuu wa Chama hicho Richard Lyimo,ambae amechaguliwa kuwa Mwenyekiti alikuwa hana mpinzani wakati katika nafasi hiyo ilikuwa na wagombea wengine .


Nae Katibu wa TLP Mkoa wa Arusha,Kinanzaro Mwanga,ambae pia alikuwa mgombea Uenyekiti taifa,amesema cha ajabu unafanyika uchaguzi ngazi ya Taifa wakati ngazi za chini haujafanyika.


Amesema kwa mjibu Katiba ya TLP toleo la 2009 inaelekeza uchaguzi uanzie ngazi za chini na utamalizikia ngazi za taifa.


Amesema kuwa kitendo hicho ni cha ukiukwaji mkubwa wa Katiba ya TLP hivyo uchaguzi huo ni batili hivyo wanamuomba Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kuufuta ili mchakato uanze upya kuanzia ngazi za chini .


Amesema kuwa kwenye Barua yao Kwa Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini imeeleza kuwa kwenye nafasi ya Uenyekiti taifa kulikuwa na wagombea watano waliopitishwa na halmashauri kuu ya Taifa,February 5 mwaka Jana kwenye kikao kilichofanyika makao makuu ya Chama hicho,Magoneni Jijini Dar es Salaam.


Amewataja wagombea hao kuwa ni pamoja na Richard Lyimo,aliekuwa Katibu mkuu taifa ambae amechaguliwa tayari kuwa mwenyekiti ambae analalamikiwa kuvunja Katiba wagombea wengine wa nafasi hiyo waliopitishwa ni Abu Chagawa,Ivan Maganza ,Stanley Ruyamgabo na Kinanzaro Mwanga ambae ni Katibu wa TLP Mkoa wa Arusha ,ambao wameeleza kwamba hawakupewa taarifa ya Mkutano mkuu wa uchaguzi hivyo hawakuhudhuria.


Barua hiyo imeeleza kwamba wajumbe wa Mkutano mkuu ni Wenyekiti na Makatibu wa mikoa yote bara na Visiwani,Wajumbe watatu wa halmashauri kuu ya Taifa  kila Mkoa  ,hivyo Jumla ya wajumbe wote ni wa Mkutano mkuu wa uchaguzi ni 185 ambapo zaidi ya robo tatu kutoka bara. na visiwani hawakuhudhuria kwa sababu ya kutopata taarifa ya Mkutano mkuu wa uchaguzi.

Post a Comment

0 Comments