SERIKALI YAMSOMEA MASHTAKA 60 YA UHUJUMU UCHUMI NA UTAKATISHANI MFANYABIASHARA NA MWEKEZAJI MZAWA ARUSHA, YAJIPANGA NA MASHAHIDI 80 NA VIELELEZO 461!

 Na Joseph Ngilisho-ARUSHA

SERIKALI imemsomea mashtaka 60 ya uhujumu uchumi ,mfanyabiashara na mwekezaji Saleh Salimu Alamry (54) Mkazi wa Njiro Jijini Arusha akikabiliwa na mashtaka ya  kuongoza genge la uhalifu, kughushi na utakatishaji fedha haramu kiasi cha dola za kimarekani milioni 8 akiwa mkurugenzi mwenza wa kampuni mbili za uwindaji na utalii ya Sunset Tarangire limited na Alrajhi Holdings LTD  

Mwingine aliyesomewa mashtaka  ni wakili wa kujitengemea Sheck Mfinanga ambaye anakabiliwa na mashtaka ya kughushi na kuwasilisha nyaraka za uongo.

Akisoma mashtaka hayo leo februari 20,2025 mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya hakimu Mkazi Arusha,Erasto Philly ,wakili wa serikali mwandamizi,Edgar Batulaki akisaidiana na Jackline Mosha na Alawi Miraji,alisema agosti mwaka jana walipata malalamiko kutoka kwa wabia wenzake Khaled Alrajhi na Abdulkarim Alrajhi raia wa nchi ya Saud Arabia.

Wakili alisema kuwa wabia wenzake kupitia kampuni yao ya Sunset Tarangire limited na Alrajhi Holdings LTD  walidai kuwa Saleh Amry ambaye ni mkurugenzi mwenza alifanya vitendo vya uhalifu kwa kupoka hisa 18 isivyo halali ikiwa ni mali ya  kampuni hizo na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Alisema mwekezaji huyo na wakili mfinanga  walikamatwa na uchunguzi ulifanyika na leo uchunguzi umekamilika na mahakama ya hakimu mkazi imefunga  mashtaka ,na mashtaka yao yataenda kusikilizwa na mahakama kuu kitengo cha rushwa na uhujumu uchumi kwa makosa yote 60.

Wakili Batulaki alisema kuwa matukio hayo yalifanyika kati ya mwaka 2019 hadi 2024 na waliyatenda katika mikoa ya Arusha,Dar es Salaam,Pwani na Manyara.

Aliieleza mahakama hiyo kuwa  ofisi yake imejipanga na kesi hiyo na imejianda kuleta Mashahidi 80,vielelezo 461 pamoja na vidhibiti 12 ambazo ni pamoja na nyumba za kuishi zilizonunuliwa na mshtakiwa Saleh Amry.

"Hadi sasa hatujashilikia mali zozote za washtakiwa labda kama zimetunzwa kwa sababu maalumu na kuhusu suala la mshtakiwa wa pili wakili Sheck mfinanga kupata dhamani katika kesi ya uhujumu ni kwamba katima uchunguzi wetu hatukukuta kosa la kumnyima dhamana"

Akiongea  nje ya mahakama wakili anayemtetea mshtakiwa wa kwanza   Mosses Mahuna na Faisal Rukaka alisema kikichofanyika leo mahakamani hapo ni kufunga shauri hilo baada ya washtakiwa kusomewa mashtaka yao na kesi hiyo kuhamishiwa mahakama kuu kitengo cha rushwa na uhujumu uchumi ambayo ndio ina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.

Alisema wao wamejipanga na utetezi wa mteja wao na wanasubiri  shauri hilo lipangiwe tarehe ya kuanza kusikilizwa  katika mahakama kuu kitengo cha mafisadi.





 



Ends...


Post a Comment

0 Comments