RC MAKONDA APONGEZA TRA KWA KUPUNGUZA MALALAMIKO YA WAFANYABIASHARA, KAMPUNI YA HANSPAUL YANYAKUA TUZO NZITO YA MLIPAKODI BORA!

 Na Joseph Ngilisho-ARUSHA


MKUU wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA mkoa wa Arusha kuendelea kufanya kazi kwa ukaribu na wafanyabiashara wa Mkoa huo na kujiepusha kuwabughudhi wafanyabiashara wanapokuwa wakikusanya kodi.

Makonda alitoa kauli hiyo katika usiku wa mlipa kodi ambapo TRA ilitoa tuzo kwa walipakodi bora ,hafla iliyofanyika katika hotel ya Mount Meru jijini Arusha.

Katika hafla hiyo Makonda alimpongeza  mfanyabiashara Kamaljit Singh  wa kampuni ya HANSPAUL AUTOMECHS LIMITED ya Jijini Arusha kwa ushirikiano mzuri na serikali katika suala la ulipaji wa Kodi"

Aidha aliipongeza TRA pia kwa kuendelea kupunguza malalamiko ya kikodi kutoka kwa wafanyabiashara.

Katika sehemu ya Hotuba yake kando ya kuisifu Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa kuvuka malengo ya ukusanyaji wa mapato kwa mwaka 2023/24,Makonda aliwataka wadau wa makusanyo ya serikali kuendelea kujenga mahusiano mazuri na walipakodi ili kuhakikisha kuwa wanakuwa sababu ya Biashara kukua badala ya kufa kutokana na sababu mbalimbali.

Moja ya waliopata tuzo za mlipaji bora ni pamoja na Kampuni ya Hanspoul  ya  HANSPAUL AUTOMECHS LIMITED ya Jijini Arusha (Automotive Ltd ) ambao wamekua  washindi wa pili ikiwa ni kwa mara nyingine wakipata tuzo ya mlipaji bora wa kodi .

Hata hivyo  Kamaljit Singh Hanspaul
Hanspaul Group Chairman wa kampuni hiyo ya hasnpoul akizungumza na vyombo vya habari  ametoa rai kwa  wananchi na wafanya biashara wengine kua na tabia ya kulipa kodi mara kwa mara kwani taifa linajengwa kwa kodi za maendeleo na sio vinginevyo.






Ends.....

Post a Comment

0 Comments