RC MAKONDA APIGA MARUFUKU DC KWENDA KWENYE MIKUTANO YA GAMBO!

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

MKUU wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda amempiga Marufuku Mkuu wa wilaya ya Arusha, Emmanuel Mkude kushiriki vikao vya Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo akidai vimejaa porojo, upotoshaji na uchonganishi.

Dc Mkude 


Akiongea wakati alipokaribishwa katika kikao maalumu cha bajeti cha Baraza la madiwani jiji la Arusha ambacho kilipitisha bajeti ya sh,bilioni 118.9 ,Makonda alimtaka Mkuu huyo wa wilaya kutoshiriki vikao vya mbunge kwa ajili ya kuhalalisha matamko yasiyo na tija .


Katika hotuba yake, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, aliwataka madiwani kuhakikisha miradi yote ya viporo inakamilika kwa wakati huku akisosotiza kupitiankauli mbiu yake kuwa "Panda miti usipande Fitina"

Alisema kuwa mbunge (bila kumtaja jina) akiwa kwenye mikutano yake aliibua wizi wa sh,milioni 252 na katika mkutano huo Makonda aliagiza kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria  watu wote wanaotuhumiwa kupanga njama za kuiba fedha kiasi cha Shilingi Milioni 252, fedha zilizotengwa kwa manunuzi ya eneo la ekari sita kwaajili ya ujenzi wa shule kwenye Kata ya Murieth Jijini Arusha.

Alisisitiza umuhimu wa Viongozi kuhudhuria vikao na kulaani tabia ya kutohudhuria vikao na kuzungumza kwenye mikutano ya hadhara yale yanayopaswa kuzungumzwa, kujadiliwa na kutafutiwa majibu ndani ya Vikao.p


"Haiwezekani miradi inapoanza maneno yanakuwa mengi ilhali wananchi wanahitaji maendeleo. Hakikisheni miradi yote viporo inakamilika kwa wakati lakini pia pandeni miti, msipande fitna," alisema Makonda.



Aliendelea kusisitiza kuwa anataka Arusha kuwa mkoa wa mfano na kwamba hatakubali kupungua kwa mapato waliyojiwekea.



"Nataka Mkoa wa Arusha kuwa namba moja kwa kila kitu. Hatuwezi kukubali kupunguza mapato, tunataka kuongeza mapato ili maendeleo yaweze kufanyika katika kila kata," alisema Makonda.

"Nimeiona hiyo taarifa ya upotevu wa fedha hizo jana zinazodaiwa kupi gwa nataka nipate majibu ,yaani nikupanga fitina tu na majungu na kama jambo huna uhakika nalo tuambie tuchukue hatua tusitukie majukwaa ya kisiasa kuleta fitina "

"Unampeleka mkuu wangu wa wilaya mahala na kwenda kufanya matamko halafu hana majibu siku nyingine usiende ,lazima ukienda kwenye mkutano uwe na uelewa wa kutosha "


Ends...


Post a Comment

0 Comments