By Ngilisho Tv
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, mwenyeji wa mkutano wa kilele wa kikanda wa kutatua mzozo wa DRC, amezitaka pande zinazohusika katika mzozo huo kushiriki kikamilifu katika mazungumzo.
"Tunatoa wito kwa pande zote zinazohusika katika mzozo wa DRC kushiriki vyema katika mazungumzo, kuweka kipaumbele kwa ustawi wa watu wake na kujitolea kuishi pamoja kwa amani."
Wakuu wa nchiChanzo cha picha,Ikulu Tanzania
Aliwataka viongozi wa ukanda huo kutafuta suluhu la mzozo huo, huku akionya kuwa iwapo watashindwa, historia itawahukumu vikali.
“Kama viongozi wa kanda, historia itatuhukumu vikali ikiwa tutanyamaza na kutazama hali inavyozidi kuwa mbaya siku hadi siku.
Na kulingana na falsafa ya suluhisho la Kiafrika kwa shida za Kiafrika, nchi zetu zina jukumu la pamoja la kuhakikisha tunashughulikia kwa haraka changamoto zilizopo za ukosefu wa usalama ambazo zimeathiri sana ustawi wa raia wasio na hatia
0 Comments