Na Joseph Ngilisho ARUSHA
WADAU wa Sekta ya Utalii wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa Maono yake ya kuanzisha Royal Tour ambayo imekuwa na matokeo Chanya katika kukuza utalii Mkoani Arusha kupitia biashara ya Mahotel.
Hayo yamebainishwa na Meneja Utawala wa hoteli ya kitalii ya PALACE, Joseph Mremi , katika hafla ya kukata na shoka ya kupongezana kwa menejimenti ya hoteli hiyo pamoja na kumuunga Mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya kukuza utalii Arusha, iliyofanyika January 31,2025 katika hoteli hiyo na kuhudhuliwa na wageni mbalimbali.
"lengo kuu la hafla hii ni kumuunga Mkono Rais wetu Samia kwa kazi kubwa anayoifanya ya kukuza utalii kupitia Royal Tour ambayo imekuwa na tija kubwa kwetu kama wadau wa Utalii"
Alisema hafla hiyo pia ililenga kuwakutanisha na wadau wengine wa utalii ambao wamekuwa msaada mkubwa katika ustawi wa hoteli hiyo katika kujenga mahusiano ya kibiashara tangu kuanzishwa kwake miaka kumi na tano iliyopita.
"lengo lingine lililotukutanisha hapa ni kubadilishana uzoefu na wadau wengine wa utalii katika kukuza biashara zetu na kuitangaza Arusha"
Mremi aliwashukuru wadau wa utalii waliojumuika katika hafla hiyo iliyoenda sanjari la kuwashukuru wafanyakazi wa hotel hiyo kwa ushirikiano wao na kuwapa zawadi .
Aliwaeleza wadau wa utalii huduma mbalimbali zinazotolewa katika hoteli hiyo ikiwa ni pamoja na huduma za Mikutano,Chakula,Mazoezi yaani GYM ,Sauna na Ateam Bath bure,kufua nguo kwa wageni kutoka nje ya hotel kwa gharama ndogo.
ends.....
0 Comments