ONA DIWANI WA CCM ALIVYOMVUA NGUO MBUNGE GAMBO,ADAI NI MZIGO HAFAI HATA KUWA BALOZI WA NYUMBA 10,AMWOMBA RADHI RC MAKONDA 'TULICHAGUA BOMU'!

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA


DIWANI wa kata ya Themi  (CCM) katika jiji la Arusha Lobora Ndarpoi,amesema kuwa Mbunge wa Arusha Mjini,Mrisho Gambo ni mzigo na hafai kuendelea kuwa mbunge wa jimbo hilo ama kuchaguliwa kuwa  kiongozi wa umma.


Diwani huyo ambaye amekuwa mwiba na mkosoaji mkubwa wa mbunge huyo hadharani, amekuwa wa  kwanza kumwomba  radhi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda kwa niaba ya wananchi akidai kuwa walikosema kumchagua na hawatarudia tena.

"Naomba niwe wa kwanza kumwomba radhi mkuu wa mkoa kwa niaba ya wananchi kwa kuwa tulimchagua mbunge wa hovyo ambaye haeleweki ,anayejiona mjuaji kuliko mtu yoyote"

"Huyu Mkuu wa mkoa Makonda ni sipesho Jifti hapa Arusha ,tumewahi kuwa na wakuu wengi wa mkoa Tangu Uhuru ,lakini hatujawai kuwa na mkuu wa mkoa wa aina hii,namwomba radhi Makonda kwa niaba ya wananchi wa jiji la Arusha wanaopenda maendeleo tulikosea sana kumchagua Gambo"

"Huyu mbunge ni kama amechanganyikiwa,haelewi anachokifanya,wewe mbunge kwenye baraza la madiwani huji,wewe mbunge kwenye kamati mbalimbali za maendeleo huji,wewe mbunge kwenye kamati ya fedha huji ,mimi nimebahatika kuwa kwenye kamati hiyo amekuja mara moja tu ,sasa huyi ni mbunge ama ni matatizo tu anatuletea"

Aliongeza kuwa Gambo aliwahi kutamka wazi kuwa hawezi kukaa meza moja na madiwani, "ina maana Gambo anaakili zaidi kuliko sisi(Madiwani)akija Mkuu wa wilaya ,mkuu wa Mkoa ,Mkurugenzi ambaye hatataka kuingia kwenye mfumo wake anageuka adui ,huyu mbunge ni mzigo tena mzigo mzito anayetukwamisha"

Alisema  "huwezi kwenda kujenga hoja barabarani kwa kutokea kama mwizi na kuongea hovyo vitu ambavyo havipo,huyu mbunge ni Komediani sio kiongozi anayeweza kutetea wananchi"

Alisema ili waweze kutatua na kumaliza matatizo ya wananchi lazima washirikiane Mkuu wa wilaya ,Mkuu wa Mkoa ,Mkurugenzi na Mbunge lakini huyu mbunge amekalia vituko tu.

"Mimi namwombea mungu amalize miaka mitano ya ubunge wake atuachie jiji letu yeye akafanye kazi ya IT hiyo ndo kazi ya taaluma yake  ,hafai kuwa kiongozi hata wa ubalozi wa nyumba kumi.

Ends...







Post a Comment

0 Comments