NMB YASHIRIKI KIBABE ZOEZI LA UPANDAJI MITI ARUSHA YAMUUNGA MKONO RC MAKONDA KUIFANYA ARUSHA YA KIJANI

 Na Joseph Ngilisho- ARUSHA


BENKI ya NMB ni miongonj mwa Taasisi za fedha  zilizoshiriki zoezi la Upandaji Miti lililozinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Paulo Makonda,katika  wilaya ya Arumeru na kuahidi kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya mkoa katika suala la utunzaji wa Mazingira.

Akiongea katika hafla hiyo iliyohusisha miti milioni 1,Makonda amezitaka mamlaka na taasisi mbalimbali mkoani hapa kuhamasisha na kushiriki utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti ili kukabiliana na tishio la mabadiliko ya tabia ya Nchi.

Aidha aliagiza mamlaka zinazosimamia  vibali vya ujenzi kuhakikisha mwombaji wa ujenzi lazima awe na eneo la Upandaji miti kabla ya kupatiwa kibali cha ujenzi.
 

Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini,Baraka Ladsilaus alisema  benki hiyo imekuwa na  kampeni  ya utunzaji wa mazingira na mwaka jana 2024 benki hiyo ilipanda miti 1000 ikiwa ni hatua moja wapo ya kuifanya Arusha ya kijani.

"Leo tumeungana na mkuu wa mkoa katika zoezi la upandaji miti na sisi kama NMB tulianza kampeni hii mwaka jana kwa kupanda miti 1000 ,NMB ni wadau wakubwa wa mazingira licha ya kutoa misaasa mingi mashuleni tutahakikisha  tunaunga mkono utunzaji wa mazingira"

Alisema Benki hiyo imeitikia wito wa mkuu wa mkoa kushiriki zoezi hilo na wao kama taasisi za fedha watahakikisha wanaunga mkono jitihada za serikali katika suala la kupanda miti na kutunza mazingira.

Alimpongeza mkuu huyo wa mkoa kwa wazo hilo la upandaji wa miti na kuomba  kuwa  zoezi hilo liwe endelevu na wao wataendelea kuunga mkono bunifu za mkuu wa mkoa zenye tija  ili kuhakikisha Arusha inakuwa ya kijani.






Ends...








Post a Comment

0 Comments