MKE AMUUA MUME ARUSHA, KISA ETI HALETI PESA NYUMBANI,WATU WALIAMSHA NA KUVUNJA NYUMBA TAZAMA HII

By Ngilisho Tv 

Mwanamke anayefahamika kwa jina la Mama Ayubu mkazi wa mtaa wa Banda mbili Kata ya Sombetini Jijini Arusha, anadaiwa amjumuua mume wake aitwae Daudi Estomii (45) ikiwa ni baada ya kuwepo kwa tuhuma za muda mrefu kuwa amekuwa akimpiga mwanaume huyo pindi anaporejea nyumbani nyakati za usiku huku akiwa hana chochote mkononi mwake.


Inaelezwa kuwa mbali na tukio hilo mwanamke huyo siku za hivi karibuni alifanya jaribio la kutaka kumnyonga mama mkwe wake kwa mtandio kutokana na kitendo cha mama huyo kutaka kuingilia kati ugomvi wa mwanae na mwali huyo.


Aidha, Inaelezwa kuwa licha ya mwanaume huyo kushushiwa kipigo mara kwa mara, hakutaka mke wake achukuliwe hatua zozote za kisheria kwa madai kuwa hawezi kumshtaki mke wake kwenye vyombo vya sheria.


Kadhalika, baada ya kuwepo kwa madai hayo wananchi wenye hasira kali wamevamia na kuvunja nyumba ya marehemu kwa madai kuwa mwanamke huyo pamoja na wanae wawili hawatakiwi kuishi katika nyumba hiyo kwasasa kwakua wote kwapamoja wanadaiwa kuhusika na mauaji hayo.

Post a Comment

0 Comments