MAHAKAMA KUU KANDA YA MOSHI KUMHUKUMU MSIMAMIZI WA MIRATHI YA MAREHEMU KYAUKA !

Na Joseph Ngilisho,ARUSHA



MAHAKAMA Kuu kanda ya Moshi, itatoa hukumu ya Kesi Maarufu ya muda mrefu ya kugombea mali za Marehemu mfanyabiashara, Paul Kyauka aliyefariki miaka 23 iliyopita ambapo msimamizi wa mirathi anadaiwa kudhulumu mali za marehemu kwa baadhi ya wanufaika .


Merehemu Kyauka alifariki mwaka 2002 na kuacha watoto 14 pamoja na wajane watatu ambao wote  ni marehemu.

Marehemu Kyauka

Hatua hiyo imekuja baada ya jaji, Safina Semfukwe wa mahakama hiyo kupokea Orodha mpya ya mali za marehemu (Inventory) na kusikiliza hoja za pande zote.

Mawakili wa upande wa walalamikaji,Matuba Nyirembe na Patrick Paul  wamepinga Orodha hiyo ya mali na kudai sehemu kubwa ya mali zimeachwa ikiwemo akaunti ya marehemu,Mashamba , nyumba ,karakana na mashine.



Wakili Paul alidai  kuwa orodha ya mali za Marehemu (Inventory)iliyowasilisha  mahakamani na msimamizi wa mirathi haikukamilika na ilijaa udanganyifu huku mali nyingi ikiwemo akaunti ya marehumu na fedha zikiwa hazipo kwenye orodha.


"Mheshimiwa Jaji kwenye orodha ya mali za Marehemu haikuonekana nyumba wala Ardhi iliyopo wilayani Rombo katika sehemu nne tofauti,ambapo katika eneo la Mengwe ,Useri  na Mrau kulikuwa na nyumba za marehemu lakini kwenye orodha tulioletewa hazimo"


"Pia katika wilaya ya Moshi  eneo la Mazinde juu kulikuwa na Prot,Mandaka Mnono kulikuwa na  shamba la  ekari 13 zote hazikuwa zimeorodheshwa kwenye orodha ya mali iliyopo mbele yako mh. jaji"




Naye wakili Matuba Nyirembe aliongeza kuwa katika orodha hiyo ya mali  hakuona  mashine tofauti tofauti za kupasua mbao pamoja na Karakana, pia plot namba 16 block M  iliyopo katika manispaa ya Moshi ambayo kumbukumbu zinaonesha iliuzwa na wasimamizi wa mirathi,Emmanuel Kyauka na Febronia Kyauka(Marehemu)  kwa mnunuzi aliyetambulika kwa jina la Mushumbuzi kwa kiasi cha sh,milioni 7.9 pia hazikuorodheshwa


"Mh jaji mali nyingi za marehemu hazikuorodheshwa kama inavyopasa kwanza hakuna ripoti ya benki ama polisi inayoonesha fedha zilichukuliwa katika akaunti ya Nairobi,tunachotaka mali zote zilizoainishwa kwenye kikao cha familia ya marehemu ziwepo kwenye orodha hii"


Hata hivyo wakili wa wajibu maombi,Daniel Ngudungi alikiri kuwa mali hizo ambazo hazikuorodheshwa zikuwa za marehemu ila baadhi alizigawa 

akiwa bado hai ,jambo ambalo lilipingwa na mawakili wa upande wa mashtaka wakidai mali hizo  zilikuwa kwenye orodha katika kikao cha  familia ya marehemu.



"Nyumba ya Mandaka Marehemu mwenyewe aligawa kwa watu watatu,Emmanuel,Peter na Chediel Kyauka  enzi za uhai wake na nyumba plot namba 16 block M iliyopo katika manispaa ya Moshi nyumba hiyo iliuzwa kwa ajili ya kulipa madeni na gharama za usimamizi"


Hata hivyo wakili Matuba alihoji kama nyumba iliuzwa kiasi cha fedha kiliwekwa kwenye akaunti gani ili kulipa hayo madeni !


Baada ya majibishano hayo Jaji Semfukwe aliahirisha shauri hilo hadi March 14,2025 saa sita mchana atatoa hukumu.



Akiongea nje ya mahakama Mmoja ya walalamikaji katika shauri hilo Richard Kyauka alidai kuridhishwa na mwenendo wa shauri hilo na kuiomba  mahakama  kutenda haki ili wanufaika wa mali za marehemu waweze kupata haki sawa kinyume na ikivyokuwa hapo mwanzo.


Ends..









Post a Comment

0 Comments