MAAFISA RASILIMALI WATU WAHIKIZWA KUTUMIA MIFUMO YA KIDIGITALI KATIKA UTENDAJI KAZI!

 Joseph Ngilisho ARUSHA 


MAAFISA Raslimali watu na utawala wamehimizwa kutumia mifumo ya  kidigitali katika utendaji kazi ili kurahisisha utendaji wao na hivyo kuondokana na mfumo wa zamani wa kutumia karatasi kujaza taarifa ambao hauna tija 


Hayo yamesemwa na Issa Sarboko Makarani,ambae ni Mkurugenzi wa mipango,Sera na Utafiti wa mafunzo ,Wizara ya mawasiliano,uchukuzi na mawasiliano Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,alipokuwa akifungua mafunzo ya kimataifa ya Maafisa Raslimali watu na utawala kutoka mataifa mbalimbali wanaokutana jijini Arusha kwenye kikao cha siku mbili.


Amesema kuwa mifumo ya utendaji kazi Ulimwengu imebadilikana mazingira ya kazi nayo yamebadilika hivyo maafisa hao hawana budi kuhakikisha wanatumia mfumo wa kidigitali Ili kurahisisha utendaji wao


Makarani,amesema kutokana na mabadiliko ya teknolojia  Ulimwenguni ,Serikali  imeamua kuendesha mafunzo hayo kwa maafisa hao ili kuwajengea uwezo na uelewa waweze kufanya kazi zao kwa kuzingatia  misingi ya kidigitali na kuonfokana na mfumo wa zamani ambao hauna ufanisi mkubwa.


Amesema mabadiliko hayo ya teknolojia tabasababisha maafisa hao kupewa mafunzo hayobili kuwa tayari kufanya kazi kisasa ilii kupata matokeo mazuri katika kazi  kwa kuhudisha mfumo wa digitali na kuwawezesha kuboreshe utendaji wao.


hayo ni kuwatayatisha wafanyakazi wa Sekta za umma Nchini  kufanya kazi  katika misingi ya kidijitali bkutokana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia inauokuwa kila kukucha.


Makarani,amesema mfumo wa sasa wa kidigitali hauna  nafasi ya mtu kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wafanye kazi kisasa kwa kutumia mitandao ambayo inarahidisha utendaji kazi na kuleta ufanisi na matokeo yenye manufaa.


Amesema wapo baadhi ya watumishi wanazembea kutekeleza majukumu yao kwa wakati lakini sasa kutokana na mfumo ya kutumia mitandao na kupata mafanikio ya haraka kwenye kazi.



Awali ,Mwenyekiti wa Taasisi ya Maafisa Raslimali watu  na utawala,(THRAPA) Christopher Kabalika Mwansasu,

amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwakusanya mameneja raslimali watu Ili kuwapa Elimu ya matumizi ya kidigitali pahali pa kazi .


Amesema Ulimwengu umebadilika Sasa mambo mengi yapo kwenye teknolojia hivyo maafisa hao ndio wanaoleta chachu ya utendaji kazi  lazima wapewe Elimu hiyo ili kuwajengea uelewa wa matumizi ya kidigitali sehemu za kazi na kufungua wigo wa uchumi wa bluu Nchini.


Mwansasu,amesema Programu hizo zina faida kubwa  hivyo wanao wajibu wa  kuwaletea Watanzania vitu mbalimbali  ili kuhakikisha utendaji wa kutumia kidigitali unapewa kipaumbele.


Amesema mfumo huo unawaunganisha maafisa hai na wenzao ili wawe na mawasiliano ya pamoja pia Viongozi wanaweza kufanya maamuzi bila kuwepo ofisini kutokana na matumizi ya mifumo ya kidigitali inarahidisha utendaji kazi.na mafunzo hayo yataleta mabadiliko kwenye Utumishi wa umma kuelewa umuhimu wa matumizi ya mfumo wa kisasa wa digital pahali pa kazi ili waweze kuboresha utendaji wao.


Amesema Programu mbalimbali za matumizi ya mfumo wa digitali na matumizi ya akili mnemba, zinafundishwa Kwa kuwa teknolojia inakuwa hivyo kuleta  chachu kwenye utendaji wao.


Amesema matumizi ya mifumo unarahisisha kuwepo mtiririko kwenye maeneo mbalimbali ya kazi na hivyo kufungua uchumi hivyo maafisa Utumishi hao lazima watambue kwamba mfumo wa digital inakuwa ni kipaumbele Kwa kuwa unamwezesha kufanya  maamuzi bila kuwepo ofisini.


Afisa Utumishi Mamlaka ya udhibiti  huduma za maji na Nishati,Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mafunda Sadiki Khamisi,amesema kikao hicho kinawaongezea ujuzi zaidi katika kutekeleza majukumu yao  kufanya kazi kwa kutumia mfumo wa digitali unarahisisha utendaji kazi.


Afisa Utumishi mwandamizi kutoka mfuko wa pembejeo ,Basuta Milanzi,amesema kuwa Dunia ipo kwenye mfumo wa dojitali  na bila mfumo hakuna kinachoweza kufanyika hivyo mafunzo hayo ni muhimu kwa kuwa yanaelejeza na kusisitiza matumizi ya mfumo wa dogijitali.


Amesema sasa kuna mifumo mingi inayotumika kurahisisha utendaji kazi tofauti na zamani walikuwa wakitumia karatadi kujaza OPRAS ili kupima utendaji wa mtumishi,lakini Sasa wanatumia mfumo kujaza na mfumo umerahisisha utendaji.


Kikao hicho kinashirikisha washiriki kutoka Tanzania,Kenya Ethiopia,Sirilanka,Pakistani na Ghana Rwanda, Somalia

Post a Comment

0 Comments