Askari wawili wa JWTZ wafariki dunia, wanne wajeruhiwa DRC.
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, limetoa taarifa kuhusu kushiriki kwake katika shughuli za ulinzi na amani chini ya Mwamvuli wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya za Kikanda ikiwemo Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Taarifa hiyo imeeleza kuwa, katika mashambulizi ya mfululizo katika maeneo ya Sake na Goma yaliyofanywa na Waasi wa M23, Januari 24 na 28, limewapoteza askari wake wawili na wengine wanne kujeruhiwa.
0 Comments