LATRA MATATANI WAKIDAIWA KUMVUNJA KIUNO DEREVA BAJAJ WAKIMFUKUZA,WANANCHI WAWAAMSHIA POPO!

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 


MAOFISA wa MAMLAKA ya Udhibiti,Usafiri Ardhini (LATRA) Mkoa wa Arusha, wanadaiwa kumvunja kiuno Dereva wa bajaj, Joseph Justine,pamoja na kujeruhiwa abiria wake wawili wakati wakifukuza bajaj iliyokuwa kwenye Mwendo.


Tukio hilo limetokea mapema leo February 6,majira ya saa saba mchana katika eneo la disemba,jijini Arusha na kuibua vurugu kubwa za wananchi kutaka kushambulia maofisa hao kabla ya askari polisi kufika na kuzima vurugu hizo.


Wakiongelea tukio hilo baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamedai kwamba maofisa hao wa LATRA ambao hawakufahamika mara moja majina yao walionekana wakifukuza bajaj hiyo yenye namba  MC 775 ECC na mmoja wa maofisa hao alionekana akidandia bajaj hiyo na kusababisha   kupinduka .

Katika tukio hilo watu watatu walijeruhiwa akiwemo dereva ambaye alivunjika kiuno pamoja abiria mmoja anayedaiwa kuvunjika mguu ambao wamelazwa katika hospital ya Mkoa Mt Meru.

Katika tukio hilo wananchi walionekana kulaani tukio hilo na kuonesha hasira ya kutaka kuwashambukia maofisa hao wa LATRA waliokuwa wameambatana na migambo wakidai kuwa ukamataji huo haukuwa na 𝙨𝙩𝙖𝙝𝙖.

 Meneja wa Latra ,Arusha, Ayubu Omari alipohojiwa juu ya tukio hilo alidai kwamba mamlaka hiyo inaendesha zoezi la kukamata Bajaji ambazo zimekuwa zikifanya kazi bila  kufuata sheria.

"Hii operesheni naifahamu na ipo kisheria, huyo dereva wakati akifuatiliwa alianza kuwakimbia maofisa wetu na kwenda kugonga ukuta "

Alisema kwa sasa dereva huyo amelazwa katika hospitali ya Mt Meru na wanasubiri apone wampandishe mahakamani.

ends





Post a Comment

0 Comments