By Ngilisho TV
Wanajeshi wasiopungua 75 leo Jumatatu watafikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuwakimbia waasi wa M23, wanaoungwa mkono na Rwanda katika Jimbo la Kivu ya Mashariki ya Kivu, na kwa vurugu dhidi ya raia, ikiwa ni pamoja na mauaji na uporaji.
Taarifa hii imethibitishwa na Ofisi ya mwendesha mashtaka wa kijeshi siku ya Jumapili, huku Umoja wa Mataifa ukiwa umetoa ripoti ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na kunyongwa, ubakaji wa genge na utumwa wa kingono ,kufuatia msako mkubwa wa M23.
Mwishoni mwa mwezi Januari ambao ulipelekea kutekwa kwa mji mkubwa wa Goma Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
0 Comments