Na Joseph Ngilisho ARUSHA
MTAALAMU na mbobezi wa Tiba asili Nchini,Dkt KAZOBA MWESIGA amewatoa hofu wananchi kufuatia tishio la Marekani kusitisha misaada ya kiafya katika nchi zote zinazosaidiwa na Marekani ikiwemo Tanzani ,akidai kuwa wamejipanga kikamilifu kutoa huduma ya tiba mbadala kwa wananchi wenye Changamoto ya Kiafya.
Dkt Kazoba ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kazoba International Herbal Products, ametoa kauli hiyo jijini Arusha katika matembezi ya kutambulisha huduma zake ikiwemo dawa mpya ya KAZO LINE inayotibu Changamoto ya maumivu ya viungo vya Mwili na vidonda vya Tumbo.
Dkt Kazoba ambaye ametunukiwa tuzo mbalimbali na serikali kutokana na Umahiri wa huduma anazotoa katika mikoa mbalimbali nchini, pamoja na nje ya nchi,amesema yupo tayari kushirikiana na serikali katika kutoa huduma za kiafya ili kukabiliana na tishio la nchi ya Marekani.
"Kwanza naipongeza serikali kwa kutambua mchango wa wataalamu wa tiba asili hapa nchini ,mimi kama mtaalamu na mtafiti wa tiba asili,nimejipanga kukabiliana tishio la Marekani la kusitisha misaada ya kiafya, wananchi wasihofu nipo tayari kushirikiana na serikali"
Alisema pamoja na ujio wa dawa mpya ya KAZO LINE inayotambuliwa na mkemia mkuu wa serikali na kusajiriwa,pia anatoa huduma ya tiba asili zaidi ya Hamsini.
"Kwa leo nipo Mkoani Arusha nimekuja na Dawa Mpya ya KAZO LINE ambayo imekuwa ikifanya vizuri katika jamii na imetambuliwa na mkemia mkuu wa serikali ,Chuo Kikuu Cha Dar es salaam na hospitali ya Taifa ya Muhimbili na nimepatiwa vyeti mbalimbali na wizara ya Afya kwa kutambua huduma zangu" Alisema
Aidha,ameziomba mamlaka zinazohusika na utoaji wa huduma ya tiba mbadala kudhibiti wimbi la matapeli wa dawa asili wanaochafua tasinia hiyo kwa kuwatapeli wananchi wenye shida za kiafya.
Dkt Kaziba atakuwepo Arusha kwa wiki nzima katika ofisi yake iliyopo eneo la Round about ya FLORIDA,akitoa tiba na ushauri .
ends .
.
0 Comments