GAMBO APIGWA TENA ARUSHA TAKUKURU KAZINI KUMCHUNGUZA NI TUKIO LA WIZI ,RC MAKONDA AAGIZA WAHUSIKA WA UPIGAJI WA SH,MILIONI 400 HADI MACHI WAPATIKANE!

 RC MAKONDA ATOA MWEZI MMOJA, TAKUKURU KUWAPATA WALIOKWAPUA MILIONI 400 ZA WAENDESHA BODABODA.

By Ngilisho Tv

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda leo Alhamisi Februari 27, 2025 ameipa mwezi mmoja Taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa TAKUKURU mkoa wa Arusha kuhakikisha wanafanya uchunguzi, kuwahoji na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wahusika wote wanaodaiwa kuiba takribani Milioni 400 zilizokuwa mali ya Umoja wa Bodaboda Mkoa wa Arusha.


Miongoni Mwa watakaohojiwa na Takukuru ni pamoja na Mbunge wa Arusha Mrisho Gambo na viongozi wa waliopita wa umoja huo.

Kauli ya Mkuu wa Mkoa imekuja kufuatia malalamiko yaliyotolewa leo, February 27,2018 na Viongozi wa Umoja huo wa bodaboda kwenye Kikao maalum cha kamati ya ushauri ya mkoa, kilichoketi leo kujadili makadirio ya mpango wa bajeti ya mwaka 2025/2026.


 Ilidaiwa kuwa mwaka 2018, wadau mbalimbali walichangia fedha hizo na kuwekwa kwenye akaunti maalum ya umoja huo na baadaye kuanza kuchotwa kupitia matawi mbalimbali ya benki na waliokuwa Viongozi wa Umoja huo huku Gambo akitajwa moja ya viongozi waliokuwa na mamlaka ya kusaini pesa kutoka .


Wakati wa kikao hicho, Katibu wa Umoja huo mkoa wa Arusha Hakim Msemo mbeke ya Wajumbe wa RCC amehoji ni kwanini imekuwa ngumu kwa watuhumiwa kukamatwa na kufikishwa mahakamani licha ya kuwa yeye binafsi amewahi kusafiri mpaka Dar Es salaam na kupata taarifa za wahusika na kisha kuzifikisha TAKUKURU lakini bado kumekuwa na kigugumizi katika kuwachukulia hatua.


 Makonda katika maelezo yake ameeleza kulifahamu suala hilo kabla hata hajawa Mkuu wa Mkoa, akitoa hadi Machi 27, 2025 TAKUKURU itoe ripoti kwa wanahabari kuhusu uchunguzi wa suala hilo na ikiwa hakutokuwa na majibu Mkoa utahitimisha kuwa baadhi ya maafisa wa TAKUKURU nao ni miongoni mwa wanufaika wa wizi huo.


Makonda aliwahoji Takukuru iwapo Gambo kama amehojiwa kuhusiana na wizi wa fedha hizo ambapo Takukuru walikiri kumhoji ingawa alitaka uchunguzi ufanyike tena pamoja na kuwahoji wanaohisiwa akiwemo mbunge huyo .



Ends..

Post a Comment

0 Comments