By Ngilisho Tv
MWANASIASA Mkongwe, Dk.Wilbroad Slaa amesema kwa sasa yupo tayari kufanya kazi kwa karibu na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kile alichoeleza kwamba kilichomuondoa katika chama hicho sasa hakipo.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoka mahakamani, ambapo ameachiwa huru baada ya kuwekwa ndani kwa siku zaidi ya 40, Dk Slaa amesema kwa sasa hana tatizo la kufanya kazi kwa karibu zaidi na chama hicho cha upinzani.
“Mimi nadhani kwa sababu kile tunachokipigania wamekiweka wazi , sasa hivi kile kilichoniondoa 2015 kimeshafutika , sina tatizo lolote kufanya kazi kwa karibu zaidi na CHADEMA kwa utaratibu wa CHADEMA” amesema Dk.Slaa.
0 Comments