CHUO CHA UHASIBU ARUSHA( IAA)CHAWANOA WAANDISHI WA HABARI WA MTANDAONI.

 IAA YAWANOA WAANDISHI WA HABARI WA MTANDAONI

By Ngilisho Tv -ARUSHA 

Chuo cha Uhasibu Arusha kimetoa mafunzo kwa waandishi wa habari za mtandaoni kuhusu Digital Journalism and Social Media Engagement pamoja na Online Journalist Personal Branding kwa lengo la kuwawezesha waandishi hao, kuboresha ujuzi wao katika uandishi wa habari, matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii kwa ajili ya kusambaza taarifa  na kujenga chapa (brand) yao binafsi kama waandishi wa habari wa mtandaoni.


Mafunzo hayo yamelenga kuwawezesha waandishi wa habari kutumia teknolojia ya kisasa katika ukusanyaji, uchakataji, na usambazaji wa habari kwa njia za kidijitali, huku wakizingatia maadili ya taaluma ya uandishi wa habari.


Akifungua mafunzo hayo Mkuu wa Chuo Prof. Eliamani Sedoyeka, amesema  kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa chuo katika kusaidia taaluma ya uandishi wa habari kidijitali ili kuhakikisha kuwa waandishi wanazingatia weledi, maadili na matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii katika kusambaza habari.


Amesema Chuo kwa kutambua mabadiliko makubwa ya Teknolojia kitahakikisha kinaendelea kuwaandaa wanafunzi katika sekta ya habari, kwa kuwapa ujuzi wa kisasa utakaowawezesha kutumia teknolojia kwa ufanisi na kujiajiri wenyewe badala ya kutegemea kuajiriwa.

Akizungumza katika mafunzo hayo Muwezeshaji sekta ya habari, Bakari Machumu, amesisitiza kuwa waandishi wanapaswa kuwa wabunifu, kutumia teknolojia kwa ufanisi  kuhakikisha wanazingatia madili ya taaluma yao na kusaidia kuimarisha taswira ya taasisi wanazofanyia kazi ili kuongeza uaminifu na ushawishi katika sekta ya habari za kidijitali.


Mafunzo hayo ya siku mbili yameanza rasmi leo katika Chuo cha Uhasibu Arusha na yanatarajiwa kufikia tamati kesho, yakiwakutanisha wataalamu wa sekta ya habari na waandishi wa habari wa mtandaoni kutoka majukwaa mbalimbali ya kidijitali









Post a Comment

0 Comments