FURAHIKA EDUCATION COLLEGE MKURUGENZI BUGURUNI MALAPA CENTER YA VETA,
P.O.BOX 20950,
DAR ES SALAAM
E-MAIL: info@furahikaeducation.ac.tz
Website: www.furahikaeducation.ac.tz
Simu No: +225 678 764 884
Tel: +255 778 074 099
REG/NACTVET/1113
Kumb na: FEC/NK/2025/001 06 FEBRUARI, 2025
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Chuo cha Furahika ni chuo kinachotoa elimu bila malipo katika kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya Sita Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kutoa mafunzo bila malipo kupitia kozi mbalimbali kama:-
Computer and ICT, Hotel management, Secretarial course, Tailoring, make up, Air ticketing and Air
hostess, Tourism, electricity n.k. Mkuu wa chuo cha Furahika anapenda kuwatangazia watanzania nafasi za kazi mbalimbali. Nafasi hizo ni kama ifuatavyo:
1.0 PERSONAL SECRETARY (NAFASI 03)
1.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kupokea na kuhifadhi nyaraka muhimu za ofisi
ii. Kuandaa na kuandika barua, ripoti na kumbukumbu za vikao
iii. Kupanga ratiba za vikao na shughuli za ofisi
iv. Kupokea wageni na kupokea simu kwa niaba ya ofisi
v. Kushughulikia mawasiliano ya ofisi kwa ufanisi
vi. Kujibu simu na kuelekeza wageni/wateja kwa wahusika
vii. Kuhakikisha eneo la mapokezi linakuwa safi na lenye mpangilio
viii. Kufanya kazi zote atakazopangiwa na mwajiri wake
1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji anatakiwa awe na cheti cha uhazili (Secretarial) kutoka katika chuo
kinachotambuliwa na serikali akiwa amefaulu somo la Shorthand (English) Hatimkato
(Kiswahili), Secretarial duties, Office practice, typing speed ya maneno 100 kwa dakika
sambamba na ujuzi wa computer kwenye Ms-Word, Ms-Excel, Internet and E-mail, Ms-
Publisher.
2.0 HOTEL MANAGEMENT INSTRUCTORS (NAFASI 03)
2.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kufundisha masomo ya uhudumu wa hotel wa hotel kwa ngazi ya cheti
ii. Kuandaa na kutekeleza mtaala wa mafunzo kwa vitendo na nadharia
iii. Kusimamia mafunzo kwa vitendo ya wanafunzi katika sekta ya hoteli
iv. Kuandaa na kufanya tathmini ya maendeleo ya wanafunzi
v. Kushiriki katika maandalizi ya mipango na maendeleo ya kozi
vi. Kuaimamia majukumu mengine atakayopangiwa na mwajiri wake
2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji anatakiwa awe na Diploma au shahada katika uhudumu wa hoteli, Utalii au fani
inayohusiana na hizo, awe ana uwezo wa kufundisha masomo ya Food and Beverage services,
Food production, Front office, Housekeeping. Mwombaji awe na uzoefu wa kufundisha walau
miaka mitatu na anaujuzi wa mawasiliano ya Kiswahili na kingereza, awe na uwezo wa
kufundisha kwa vitendo na nadharia kwa kutumia teknolojia za kisasa darasani. Awe amesoma
chuo kinachotambulika na serikali.
3.0 MHASIBU (01)
2.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuweka kumbukumbu za kifedha na kuhakikisha usahihi wa taarifa za fedha
ii. Kutayarisha na kufanya ulinganifu wa taarifa za mapato na matumizi
iii. Kusimamia mchakato wa malipo na mapokezi ya fedha
iv. Kutoa taarifa za kifedha kwa uongozi wa chuo
v. Kufanya marekebisho ya makosa ya kifedha na kuhakikisha mifumo ya uhasibu inafanya
kazi ipasavyo
3.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji anatakiwa kuwa na cheti cha uhasibu (CPA,ACCA) au shahada katika uhasibu au
fani inayohisiana, awe ana ujuzi wa kutumia computer katika program za uhasibu na ofisi
(QuickBooks, Ms Excel n.k) Awe amesoma chuo kinachotambuliwa na serikali
SIFA ZA JUMLA
i. Waombaji wote lazima wawe watanzania wenye umri usiozidi miaka 30
ii. Waombaji wote wanatakiwa wawasilishe barua zenye saini
iii. Waombaji wote wanatakiwa wawaambatanishe taarifa za maendeleo ya kazi (curriculum
Vitae) zenye namba ya simu na Email inayotumika
iv. Waombaji anatakiwa aambatanishe vyeti vyake vya masomo, cheti cha kuzaliwa na
kitambulisho cha Taifa
JINSI YA KUTUMA MAOMBI
Tuma barua ya maombi, nakala za vyeti vya kitaaluma, Cheti za kuzaliwa, nakala ya
kitambulisho cha Taifa na wasifu binafsi (CV) kupitia barua pepe info@furahikaeducation.ac.tz
Maombi yote yaelekezwe kwa:-
Mkuu wa Chuo,
Chuo Cha Furahika
Buguruni Malapa near St. John’s
S.L.P 20950
DAR ES SALAAM
KWA MAWASILIANO ZAIDI: +225 678 764 884
NB: Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 14 februari, 2025
0 Comments