CCM ARUSHA YATOA TAMKO ZITO, YARIDHISHWA NA KASI YA RAIS SAMIA, UTEKELEZAJI WA ILANI .

 CCM ARUSHA WARIDHISHWA NA KASI YA RAIS SAMIA, UTEKELEZAJI WA ILANI 2020/25.

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Arusha kimeunga mkono azimio la Mkutano mkuu wa Chama hicho tawala la kumuidhinisha Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania na Dkt. Hussein Mwinyi wa Zanzibar kuwa wagombea Urais kwenye uchaguzi Mkuu ujao, wakisema wameridhishwa kikamilifu na utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM ya Mwaka 2020/2025.

Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha Ndugu, Dadi Musa Matoroka leo Jumamosi Februari 01, 2025 kwenye viwanja vya Kilombero Jijini Arusha, amewaambia wakazi wa Mkoa wa Arusha kuwa serikali ya awamu ya sita imeimarisha kikamilifu sekta ya utalii, Elimu pamoja na huduma nyingine za Kijamii, suala ambalo limechochea na kukuza uchumi na ubora wa huduma hizo muhimu kwa wakazi wa Arusha.


Matoroka ametolea mfano huduma za Umeme, akisema ndani ya miaka minne ya uongozi wa Rais Samia, Vijiji vyote 392 vya mkoa wa Arusha vimefikiwa na huduma hiyo, Huduma ya Maji ikifika vijijini kwa asilimia 75 kulinganisha na asilimia 85 za Ilani ya CCM, huku Mijini huduma hiyo ikifikia asilimia 75 sawa na Ongezeko la asilimia 10 zilizoainishwa kwenye ilani ya CCM.


Kufuatia hali hiyo, Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha amewasihi wananchi wenye sifa kutoa shukrani kwa Rais Samia kupitia maboksi ya kura ifikapo Oktoba mwaka huu, kwa kuhakikisha wanampa kura za Ushindi ili aweze kutekeleza tena ilani ya CCM kwa mwaka 2025-2030.





Post a Comment

0 Comments