Na Joseph Ngilisho ARUSHA
UMOJA wa Walimu wa Shule ya Msingi Engosingiu iliyopo jijini Arusha wameamua kujitokea sehemu ya mshahara wao na kuchangishana kiasi cha sh,milioni moja ili kuwasaidia wanafunzi wao ambao wazazi wao hawana uwezo wa kuwanunulia vifaa vya shule yakiwemo Madaftari na sare za shule.
Akiongea katika hafla ya kukabidhi msaada huo kwa wanafunzi hao,ambao ni Masweta, Daftari, Kalamu,Sukari na Sabuni ,mwenyekiti wa umoja huo Mwalimu, Musa Singo ,alisema msaada huo unalenga kumsaidia mtoto kuweza kujiamini na kufanya vizuri katika masomo yake na kuwataka wadau wengine wa elimu kuguswa na hitaji la wanafunzi kama hao na kuwasaidia.
"Sisi kama walimu tuligundua kwamba baadhi ya wanafunzi wetu hawana vifaa vya kujifunzia na wazazi wao hawana uwezo, ndipo tulipoguswa na hali hiyo na kuamua kuchangishana tukapata sh,Milioni 1 na kwenda kununua mahitaji hayo kama madftari,Kalamu,Sukari , Masweta na sabuni ili ziwasidie na wajisikie kama wenzao "
Awali mwalimu Mkuu wa shule hiyo ya Engosingiu,Ramadhani Kiluvya alisema kuwa katika shule hiyo yenye wanafunzi zaidi ya 2100 wapo wanafunzi ambao wanaishi katika mazingira magumu kutokana na familia zao kutokuwa na uwezo na hivyo walianzisha utaraibu wa kuchangishana na kuamua kuwasaidia ili kuwaongezea ari ya kusoma.
"Kwa kuanzia tumewapatia msaada huo wanafunzi 40 na tutaendelea kuchangishana na tunawaomba na wadau wengine kutuunga mkono ili kuwasaidia wanafunzi ambao wanaishi katika mazingira magumu"
Naye mwenyekiti wa kamati ya shule, Paskari Mollel aliwashukuru walimu kwa hatua hiyo ya kujitolea kwani nijambo ambalo halijazoeleka ila aliwaomba wadau wengine wa elimu kuwekeza katika sekta hiyo kwa kuwasidia watoto wenye uhitaji.
Kwa upande wake Hadija Mollel katibu wa mazingira na elimu ccm, pamoja na mwenyekiti wa mtaa wa Engosingiu,Jackline Munisi waliwapongeza walimu hao kwa msaada huo na kueleza kuwa watakwenda kuhamasisha wazazi kuwapatia mahitaji ya muhimu watoto ili kupunguza utoro mashuleni.
ends..
0 Comments