YAS YATIA TIMU KANDA YA KASKAZINI, YATAMBULISHA MABADILIKO NA HUDUMA ZAKE KWA KISHINDO ARUSHA NI MWENDO WA 5G TU!

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 


KAMPUNI ya Mawasiliano Tanzania (Yas)imeendelea kutambulisha mabadiliko yaliyotokea katika kampuni hiyo pamoja na huduma zake kwa kanda ya Kaskazini baada ya kufanya mabadiliko ya Chapa yake mpya (Yas) ambayo awali ilijulikana kama Tigo.
 
 

Akiongea na waandishi wa habari mapema leo January 16,2025 jijini Arusha, Afisa Mkuu wa Biashara Yas,Isack Nchumba alisema tangu mabadiliko hayo yafanyike Novemba 26,2024 kampuni hiyo imekuwa na mwendelezo wa kutambulisha chapa yake mpya inayoenda sanjari na maboresho makubwa katika ulimwengu wa kidigitali unaotoa matumani Mapya.

"Tupo hapa Kutambulisha Mabadiliko ya Chapa yetu ya Yas, Kama mnavyofahamu Novemba 26 Mwaka jana 2024, kampuni yetu iliyofanyakazi kwa zaidi ya miaka 30 ilikuwa ikitumia jina la Tigo pamoja na Tigo Pesa, tumefanya mabadiliko hayo na sasa ni Yas na Tigo Pesa Ni Mixx by Yas"

Alisema mabadiliko hayo ya Chapa ya Yas ni hisia chanya yenye matumani mapya kwa wateja kutokana na uwekezaji mkubwa wa Mtandao Tanzania ambapo kwa sasa Yas inapatikana nchi nzima kwa Mtandao mpana wenye kiwango cha masafa ya 4G na 5G ukiwa ni Mtandao bora zaidi kwa huduma unaotambuliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA.

"Kwa miaka miwili tumepata Tuzo ya kuwa Mtandao bora kwa viwango,tunapatikana kwa sehemu nyingi zaidi Nchini na TCRA imetutambua kama watoa huduma bora katika kipindi cha Miezi tisa, hivyo chapa yetu imebadilika ili kuweza kuakisi mabadiliko chanya"
Alisema mabadiliko hayo hayatabadilisha gharama za vifurushi ,utoaji wa huduma au bidhaa zao,wateja wataendelea kununua vifurushi vyao pendwa kwa gharama zilizozoeleka,ispokuwa mabadiliko hayo yataongeza ubunifu,kuwekeza kwa vijana ,kutoa huduma bora zenye viwango vya kimataifa pamoja   na kuboresha uzoefu wa kidigitali.

Wakati huo huo, Mainoya ameongeza kuwa kampeni ya “magifti ya kugift” bado inaendelea huku washiriki wakiendelea kujishindia zawadi za kila siku na kila wiki ikiwemo zaidi ya sh, milioni 156 na simu janja 172 zilizobakia.


Awali Kaimu Mkurugenzi  kanda ya Kaskazini, Daniel Mainoya alisema Yas Kanda ya Kaskazini imejipambanua Katika mageuzi ya kidigitali Tanzania kutoa huduma bora kwa wateja wake zitakazoenda sambamba na mabadiliko hayo makubwa ya chapa Yas.

Alisema Yas Katika kipindi cha Miaka miwili mfululizo imetunukiwa tuzo ya kimataifa kama mtandao wenye kasi zaidi nchini  wenye minara maeneo mengi zaidi yenye kusoma 4G na 5G.

"Kwa sasa tunateknolojia zote tano 2G,3G,4G na 5G ambapo 5G  ndio Teknolojia ya mwisho yenye kasi kubwa kwa sasa ,ukienda Moshi utakutana na 5G,Ukienda Babati utakutana na 5G ,pia tumetanua wigo maeneo ambayo hatukuwepo ,mfano Longido, Loliondo, Lengijave, Simanjiro na maeneo mengi ya kanda ya Kaskazini utakuta Yas ipo kwa kasi zaidi"Alisema.

Ends....














Post a Comment

0 Comments