By Ngilisho Tv
WATU 10 wamefariki dunia na wengine 11 kujeruhiwa baada ya breki la lori lililokuwa limebeba saruji kushindwa kufanya kazi na kugonga watu waliokuwa wakiangalia ajali ya gari dogo aina ya Tata katika kijiji cha Chang’ombe, kata ya Segera, wilayani Handeni, mkoa wa Tanga.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Batilda Burian, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na amesema kuwa tukio hilo limetokea wakati wakijaribu kuwasaidia majeruhi wa ajali ya awali.
Kwa mujibu wa taarifa, lori hilo lenye namba za usajili T 680 BQW, likiwa linatokea Tanga limeparamia watu waliokuwa pembezoni mwa barabara na kusababisha vifo vya watu 10 papo hapo.
Mkuu huyo wa Mkoa ametoa pole kwa familia za marehemu na kuwatakia nafuu ya haraka majeruhi wote.
Aidha, ametoa wito kwa madereva na wamiliki wa vyombo vya moto kuhakikisha magari yao yanakuwa katika hali nzuri ya kiufundi ili kuepusha ajali za namna hiyo.
Ends..
0 Comments