WASIRA YUMO TENA AWAMU YA SITA ATEULIWA MAKAMU MWENYEKITI MPYA WA CCM TAIFA.

 

By Ngilisho Tv -DODOMA


Mwanasiasa mkongwe aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika Serikali na CCM, Stephen Wasira ameteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho (Bara).


Wasira ambaye jina lake limewasilishwa mbele ya mkutano mkuu wa CCM unaoendelea jijini Dodoma leo Januari 18, 2025, limepata baraka za Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Abdulrahman Kinana aliyetangaza kupumzika miezi mitano iliyopita.



Kinachoendelea sasa jina la Wasira litapigiwa kura na wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM.

Post a Comment

0 Comments