Uwanja wa ndege wa Arusha kuanza kufanya kazi kwa masaa 24 kuanzia Julai 2025.
By Ngilisho Tv-ARUSHA
Uwanja wa ndege wa Arusha unatarajiwa kuanza kufanya kazi kwa masaa 24 ifikapo julai mwaka huu 2025 ikiwa ni baada ya kukamilika kwa mradi wa kuweka mfumo wa taa unaojulikana kama Aeronautical Ground lighting (AGL) katika uwanja huo.
Hayo yamebainishwa na,kaimu mkurugenzi wa uwanja huo, Zalia Msangi katika kipindi cha Wekeza Tanzania, ambapo amebanisha kuwa kukamilika kwa mradi wa Taa za AGL kutauwezesha uwanja huo kuwa na safari za usiku na mchana.
Kukamilika kwa mradi huo kunatazamiwa kuwa chachu ya ongezeko la abiria wanaoingia na kutoka katika uwanja huo ambapo hadi kufikia sasa uwanja huo umetajwa kuwa na jumla ya miruko ya ndege 150 kwa siku katika kipindi cha "High season", na miruko zaidi ya 90 kwa siku katika kipindi cha kawaida.
Idadi hiyo inauwezesha uwanja huo kuwa ni wa pili Tanzania Bara kwa kuwa na idadi kubwa ya miruko ya ndege kwa siku huku nafasi ya kwanza ikiwa ni uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam.
Ends....
0 Comments