UKWELI WA VIJANA 170 WA KULUNA KUUAWA KWA KUPIGWA RISASI HADHARANI DR CONGO

 UKWELI WOTE SABABU ZA VIJANA 170 KULUNA KUUAWA CONGO DR

By Ngilisho Tv

Kinshasa. Serikali nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inadaiwa kuwaua vijana 170 waliokamatwa kwa madai ya kuwa wanachama wa makundi yanayotekeleza uhalifu wa mjini maarufu kama “Kuluna.” 


Vyombo vya Habari vya ndani Congo vinawaonyesha vijana hao wakiwa wamefungwa pingu mikononi huku wakibubujikwa machozi wakati wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Sheria wa taifa hilo, Constant Mutamba.


Shirika la Kimataifa la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International limeripoti kuwa mamlaka za usalama nchini humo zimewakamata watuhumiwa zaidi ya 1,400 wa uhalifu huku wakitajwa kuwa ni wanachama wa Kundi la Kuluna.


Amnesty International pia imesema kuwa kati ya waliokamatwa wengi wao ni vijana wenye umri kati ya miaka 18 hadi 35 ambao wanadaiwa kutenda makosa ya uhalifu ikiwemo uvamizi wa makazi na mauaji ya raia.


Shirika la Habari la Associated Press limeripoti kuwa vijana takriban 170 kati yao wameshahukumiwa adhabu ya kifo na tayari taarifa zinadai kuwa vijana hao wameshauawa kwa kupigwa risasi nchini humo.


Vijana hao walikamatwa kupitia Opereshezi za usalama zilizofanyika eneo la Ndobo, Lingala kwa lengo la kuwakamata vijana hao kati ya Desemba zikiongozwa waziri, Mutamba zililenga kukomesha magenge ya wahalifu katika Mji wa Ndobo wenye wakazi zaidi ya milioni 15.


Shirika la Habari Associated Press limeripoti kuwa vijana hao walihamishwa kwa makundi makundi kutoka katika Gereza lililoko Jijini Kinshasa kwenda katika gereza lililoko mafichoni na lenye ulinzi wa hali ya juu kwa ajili ya kwenda kuuawa.


Kwa mujibu wa Waziri wa Sheria nchini Congo, Mutamba, wafungwa 70 kati yao walisafirishwa siku ya Jumapili huku wengine 102 wakipelekwa katika gereza la Angenga lililopo Kaskazini mwa Jimbo la Mongala nchini humo.


Mutamba alisema vijana wote wa Kuluna walikutwa na hatia ya kufanya uhalifu wa mijini ‘urban bandits’ na wana umri kati ya miaka 18 hadi 35, japo hakuweka wazi ni lini vijana hao watauawa.


Baadhi ya raia wa Congo DR wamepongeza uamuzi huo kwa kile wanachosema itasaidia kupunguza hofu iliyoibuliwa na matukio ya vijana hao huku wengine wakihofia kuwa kutekelezwa kwa adhabu ya kifo dhidi ya vijana hao kuwa ni ukatili na uvunjaji wa haki za binadamu.


INAENDELEA SEHEMU YA 2

Post a Comment

0 Comments